Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Questions from Hon. Sheila Edward Lukuba (1 total)

MHE. SHEILA E. LUKUBA aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga mfereji mkubwa kuelekeza maji Mto Ngerengere ili kunusuru wakazi wa Kata ya Kihonda na Lukobe kwa mafuriko?
NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Sheila Edward Lukuba, Mbunge wa Viti Maalumu kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kata za Kihonda na Lukobe katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro zimekuwa zikiathiriwa na mafuriko ya mara kwa mara nyakati za mvua. Ili kutatua changamoto hiyo, Serikali imepanga kujenga mifereji ili kuyaelekeza maji katika Mto Ngerengere. Serikali imeunda timu ya wataalamu kwa ajili ya kufanya tathimini na kuandaa andiko la mradi ambalo litaonesha mahitaji halisi na njia nzuri ya kulifanyia kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, timu ya tathimini inatarajia kukamilisha kazi hiyo kabla au ifikapo Septemba 2026. Ahsante.