MHE. SALUM KHAMIS SALIM: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa majibu ya Naibu Waziri, lakini kwa sababu suala la tembo katika Wilaya ya Meatu na Jimbo la Meatu limekuwa ni la siku nyingi na mkakati wake ni huu huu kila siku, na majibu ni hayo hayo, je, Mheshimiwa Naibu Waziri haoni kwamba, kuna sababu ya kuwa na azma kubwa ya kuwaondoa tembo ambao wanaishi maeneo ya watu kwa sasa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninaomba kumpongeza sana Mheshimiwa Salum kwa kuwa na yeye sasa ni sehemu ya hifadhi na anashirikiana na taasisi zetu katika kuhami jamii yetu dhidi ya wanyama hawa wakali na waharibifu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nijibu maswali yake yote mawili kwa pamoja. Ninaomba kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri nitoe maelekezo kwa Kamishna Mkuu TAWA na TANAPA kwa kushirikiana na halmashahuri zetu kote nchini waende kuwaondoa wanyama hao ambao wapo katika makazi ya watu na katika mashamba yao. (Makofi)
MHE. SALUM KHAMIS SALIM: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza. Kwenye Jimbo langu la Bububu kumejengwa kituo cha ghorofa kwa kuzingatia matumizi ya eneo husika kabla ya uhuru. Je, ni kigezo gani kilichotumika kujenga nyumba ya chini ilhali matumizi yamekua na pia unyeti wa eneo?
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamshukuru sana Mheshimiwa Salum Salim, Mheshimiwa Mbunge ambaye amesema kwamba, kwenye jimbo lake kumejengwa kituo cha Polisi kabla ya uhuru na ni cha ghorofa. Sasa, anataka kujua ni kigezo gani kilichotumika kujenga nyumba ya chini badala ya ghorofa kama ambavyo kwa wakati huo vituo vimejengwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nyumba za makazi kwa ajili ya Askari ni moja kati ya hitaji kubwa tulilonalo katika Jeshi la Polisi pamoja na vyombo vingine vya ulinzi na usalama. Tunakiri kwamba kadiri siku zinavyoendelea na ongezeko la idadi ya watu linakua kubwa na matumzi ya ardhi yanazidi kuwa makubwa. Hivyo, inapendekezwa na kushauriwa kwamba, kadiri iwezekanavyo, tujenge nyumba za ghorofa badala ya nyumba za chini kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge amesema.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ya hali ya kibajeti na kwa mujibu wa uharaka na uhitaji wa makazi katika eneo hilo, ndiyo sababu kuu inayosababisha kujenga nyumba za chini katika baadhi ya maeneo. Vilevile kuendelea na ujenzi wa nyumba za ghorofa kwenye yale maeneo ambayo tayari fedha zipo, na pia kule ambapo wamekosa maeneo ya kujenga nyumba za chini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, katika Mkoa wetu wa Dodoma hapa tulipo, tayari tunaendelea na ujenzi wa zaidi ya nyumba sita za ghorofa kwa ajili ya makazi ya Askari. Kabla ya ukoloni kulikuwa kuna nyumba za chini ndogo ndogo ambazo hazina hadhi na hali nzuri. Kwa hiyo, kazi ya ujenzi wa nyumba za ghorofa inaendelea nchi nzima kwa kadiri ya hali ya fedha, kwa maana ya bajeti, itakavyoruhusu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha.