Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions from Hon. Condester Michael Sichalwe (1 total)

MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi. Pamoja na kuwa na sera nyingi, ipo pia sera ya watoto chini ya miaka mitano, kutibiwa bure na sera hii haijawahi kutekelezeka hata kidogo. Katika majibu ya msingi ya Naibu Waziri, yanasema ametoa takwimu ya wamama wajawazito, kwamba wakiwahudumia wote haitawezekana...

SPIKA: Mheshimiwa uliza swali.

MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Spika, swali, sasa kama takwimu ya watu wanaopaswa kuhudumiwa ni wengi, watoto na akina mama wajawazito, kwa nini Serikali isitoke kuwaambia wananchi kwamba sera hizi hazipo ili waelewe kwamba hakuna bure kwa wajawazito wala hakuna bure kwa watoto chini ya miaka mitano? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, labda tu nimwambie Mbunge namuelewa sana, ila hata yeye kwenye mipango yake ambayo ameipanga, anaianza anapanga mpango mzima, lakini anautekeleza hatua kwa hatua na nimwambie tu kwa maana ya exemption, kwa maana watu waliotibiwa na yeye mwenyewe anajua jinsi tumepambana na yeye kwenye hospitali yake ya rufaa kule Mbeya, kwa maana ya watu wa exemption kwa mwaka tu Serikali inatumia zaidi ya shilingi bilioni 667, lakini ukweli ukikuta waliohitaji exemption ni zaidi ya hao lakini pasingekuwepo na hiyo sheria pia hawa tuliyowasaidia shilingi bilioni 667 pasingekuwepo na namna ya kutekeleza.

Kwa hiyo, sheria ipo ila ni ukweli kwamba haijatekelezwa kwa 100% lakini siku zote unaweza ukapanga mipango, lakini bajeti ya kutekeleza kwa 100% inaweza isipatikane lakini ukitekeleza kwa 60% nayo ni utekelezaji, ni kujipanga kumalizia 40%. (Makofi)