Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Questions from Hon. Subira Khamis Mgalu (1 total)

MHE. SUBIRA K. MGALU aliuliza:-

Je, lini Mradi wa Maji wa Mto Rufiji utaanza baada ya upembuzi yakinifu kukamilika?
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI K.n.y. WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante, Serikali inaendelea na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa mradi mkubwa wa kutoa maji Mto Rufiji ambao utanufaisha wakazi wa Mikoa ya Lindi, Pwani na Dar es Salaam. Usanifu huo unatarajiwa kukamilika ndani ya mwaka wa fedha 2024/2025 na Serikali itaanza kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi huo. (Makofi)