Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions from Hon Maryam Azani Mwinyi (2 total)

MHE. MARYAM AZAN MWINYI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa swali dogo la nyongeza.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuzindua Awamu ya Tatu ya Mpango wa Kaya Maskini hapa nchini? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Maryam Mwinyi kuwa Serikali kwa sasa imekamilisha, tuko hatua ya mwisho kabisa ya kwenda kuanza Mpango wa Awamu ya Tatu ya Kunusuru Kaya Maskini na mpango huo uko kwenye hatua za mwisho kuhakikisha kwamba tunakwenda kutekeleza ili utekelezaji uanze kwa haraka. Mpango huu wa awamu ya tatu, ni kwenda kuboresha yale mapungufu yaliyojitokeza kwenye awamu ya pili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali tayari imeshakamilisha, ni utekelezaji unakwenda kuanza hivi karibuni.
MHE. MARYAM AZAN MWINYI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, watoto wengi wanaopata mimba za utotoni ni wale watoto ombaomba wa mitaani, je, Serikali ina mkakati gani wa kuwalinda watoto hawa?
NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE WA MAKUNDI MAALUM: Mheshimiwa Spika, Serikali ina mpango na ina mkakati wa kuwalinda watoto hawa kwa kuwafuata na kuwahoji baadaye baada ya kuwahoji kwa kuwakutanisha na wazazi wao ili waendelee na maisha na wazazi pale wanaposhindwa basi Serikali ina vituo vyetu vya kulelea watoto ambapo vipo Dodoma, lakini vipo Dar es Salaam na watoto hao wanalelewa na kupata stahiki zote kuanza elimu mpaka wanapokuwa na kutimiza miaka 18 na kuendelea na maisha yao, ahsante.