Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions from Hon. Othman Maulid Suleiman (1 total)

MHE. OTHMAN MAULID SULEIMAN: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nilikuwa ninaomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhamasisha wananchi kuweza kuzipenda na kuzinunua bidhaa zinazozalishwa Tanzania, nikiwa na maana ya kununua bidhaa za Tanzania kwanza? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili, je, Serikali haioni haja ya kuanzisha programu hii ya kizalendo kwa umma ili ipate mwamko wa kuzipenda bidhaa zetu na kuzinunua? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba niungane na Mheshimiwa Mbunge kwamba jukumu la kukuza, kuendeleza na kuhamasisha bidhaa zetu za ndani ni jukumu letu Watanzania wote. Wizara ya Viwanda na Biashara chini ya maelekezo ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Taasisi ya TanTrade tunaendelea kufanya mradi mkubwa wa branding wa bidhaa ambazo zinatengenezwa Tanzania maarufu kama Made in Tanzania Brand.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, pamoja na hayo kupitia miradi mbalimbali ya uendelezaji wa viwanda, tunaendelea kutoa hamasa kwa Watanzania na mwamko sasa hivi umeendelea kuwa mkubwa hasa kwa viongozi wa Serikali na taasisi binafsi ambao tunaendelea kuona wakivaa ama wakitumia bidhaa za Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo, ninaomba kutoa rai kwa sisi Wabunge kuendeleza hamasa yaku-promote bidhaa zetu za ndani kwa kuzitumia na kuonesha Watanzania kwamba bidhaa zetu zina ubora, zinakidhi viwango na tunazipenda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha.