Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions from Hon. Nassor Said Nassor (1 total)

MHE. NASSOR SAID NASSOR MAROO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa nafasi ya maswali ya nyongeza. Je, Mheshimiwa Wizara imetenga kiasi gani cha bajeti katika kushughulikia suala hili hasa la tabianchi?

Mheshimiwa Spika, swali la pili. Je, Mheshimiwa Waziri yuko tayari kuongozana na mimi kwenda katika Jimbo langu la Chake Chake kuziangalia hizo athari za tabianchi?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa ikitenga fedha za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kupitia bajeti za sekta mbalimbali ndani ya Serikali ikiwemo bajeti ya maji kwenye kilimo, kwenye miundobinu, kwenye nishati, kwenye misitu ambayo matokeo yake kwa ujumla yanatufanya tuweze kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Mheshimiwa Spika, kwa kule Pemba mwaka 2024/2025 Serikali ilipeleka fedha shilingi milioni 300 kwa ajili ya kujenga kuta za kuzuia athari za maji zinazotokana na bahari kwenye ufukwe wa Sipwese huko Pemba na mwaka uliofuata 2025/2026, Serikali imepeleka shilingi milioni 392 kukamilisha ujenzi wa ukuta huo.

Mheshimiwa Spika, hivi sasa ukuta huo umefikia 95% kwenye mwaka huu wa fedha. Kwenye bajeti itakayosomwa leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, itaeleza kiwango kilichotengwa kwenye eneo hili Jimbo la Chake Chake.