Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Questions from Hon. Dr. Pius Stephen Chaya (1 total)

MHE. DKT. PIUS S. CHAYA aliuliza:-

Je, kuna mpango gani wa kurasimisha viongozi wa nyumba kumi (mabalozi) kama sehemu ya kuimarisha usalama wa raia?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wa ulinzi na usalama katika ngazi ya msingi kwa maendeleo ya Taifa. Aidha, usalama wa raia umeendelea kusimamiwa na vyombo vya usalama kwa kushirikiana na wananchi kupitia mfumo wa uongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa katika ngazi za msingi ikiwemo Wenyeviti wa Vijiji/Mitaa, Vitongoji na Mabalozi. Serikali itaendelea kuboresha mfumo wa utambuzi na usalama katika ngazi ya msingi kwa kupitia mfumo wa uongozi wa Serikali za Mitaa uliopo ili kuongeza ufanisi katika kuimarisha masuala ya usalama, ahsante.