Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions from Hon. Issa Ally Mchungahela (1 total)

MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa issue ya fidia, maeneo ya Yombo katika Wilaya ya Bagamoyo, wamekaa kwa muda mrefu sana pasipokulipwa fidia. Ni lini watu hawa watalipwa fidia ikiwa maeneo haya yamechukuliwa na Serikali kwa muda mrefu? (Makofi)
WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimpongeze Mheshimiwa Mchungahela, kwa kuuliza eneo la Bagamoyo. Kubwa zaidi naomba nikuhakikishie kwamba, ni mpango wa Serikali kuhakikisha eneo la Bagamoyo linaenda kuwa nyeti kwa Taifa letu katika mpango mkakati wa viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maana yake ni katika mpango huo kuna maeneo mengine yamelipwa fidia na maeneo mengine hayajalipwa. Namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba sasa hivi amesikia Waziri wa Mipango alikuja na mpango mkakati mkubwa sana wa suala zima la ujenzi wa viwanda na hasa upande wa Bagamoyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niwahakikishie wale ambao hawajalipwa fidia, provided kwamba wapo katika taratibu zile ambazo zimeainishwa na Serikali, kila mtu atapata haki yake ile inayostahili. Ahsante sana. (Makofi)