Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Questions from Hon. Faraji Buriani Nandala (1 total)

MHE. FARAJI B. NANDALA aliuliza: -

Je, lini Wananchi wa Kata za Chikukwe, Chigugu, Chikundi, Mwena, Ndanda na Nanganga ambao wamepitiwa na Mradi wa Grid ya Taifa watalipwa fidia?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Nishati, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Faraji Buriani Nandala Mbunge wa Ndanda, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka huu wa fedha wa 2025/2026 Serikali imetenga bajeti kwa ajili ya malipo ya fidia yenye thamani ya shilingi bilioni 5.1 kwa wananchi 1,730 wanaopisha njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovoti 220 kutoka Masasi hadi Mahumbika. Hivyo, naomba kumjulisha Mheshimiwa Mbunge kuwa fidia hii italipwa mwaka huu wa fedha kadri itakavyopatikana.
MWENYEKITI: Mheshimiwa Faraji Buriani Nandala.