Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027

Hon. Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vwawa

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027

MHE. JAPHET N. HASUNGA: Mheshimiwa Spika, ninayo heshima kubwa ya kumpongeza sana Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kazi kubwa anazoendelea kuzifanya katika kujenga miundombinu ya barabara na madaraja. Kipekee nimpongeze sana kwa uamuzi wake wa kuwapatia kazi wakandarasi wanawake ili kujenga Barabara ya Luanda Nyimbili kilometa 20 katika Wilaya ya Mbozi na Mkoa wa Songwe. Wakandarasi hawa wamefanya kazi kubwa na wanaendelea kufanya kazi nzuri sana katika ujenzi wa barabara hiyo.

Mheshimiwa Spika, kilometa 20 kwa wakandarsi 12 (joint venture) ni chache sana. Lengo ni kuwajengea uwezo wa kiuchumi na uwezo wa kujenga barabara. Hivyo ni muhimu Serikali ikaona uwezekano wa kuwaongezea eneo la kilometa 40 ili kila mkandarasi awe amejenga angalau kilometa tano. Chini ya kilometa tano wanaweze wasipate faida na kujenga uwezo wa kiuchumi.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa wanafanyakazi nzuri ni vizuri wakaongezewa kilometa zaidi kwani wameonesha uwezo mkubwa sana wa kazi na kwa viwango vya kimataifa. Wanawake wanaweza. Hongera sana Mheshimiwa Rais na Waziri wa Ujenzi kwa kazi kubwa.

Mheshimiwa Spika, ili kuwavutia wakandarasi hawa wanawake ni muhimu mkatoa motisha kuwa mkandarasi atayekuwa wa kwanza kumaliza kazi kwa viwango vinavyokubalika basi atapewa kilometa 20 zaidi ili aendelee na kazi.

Mheshimiwa Spika, pia Mheshimiwa Waziri naomba Serikali iangalie uwezekano wa kuanza ujenzi wa mizani pale Iboya ili kupunguza foleni ya pale Tunduma na kuwafanya wafanyabiashara kutumia muda mfupi zaidi ili kupunguza gharama za uendeshaji wa biashara.