Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027

Hon. Eng. Mwanaisha Ng'anzi Ulenge

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Spika, Sera ya Ujenzi ya mwaka 2013 ilitambua ushiriki wa wanawake katika kazi za barabara na ni muda mrefu Wizara imekuwa ikiwezesha kufanyika kwa mafunzo kwa wakandarasi wanawake na wakandarasi wa madaraja ya labour based wamekuwa wakipata kazi ndogo ndogo.

Mheshimiwa Spika, matokeo makubwa ya wakandarasi wanawake kutekeleza barabara ya lami imetokea wakati huu ambao tuna Rais mwanamke. Tunaipongeza Serikali kwa kutenga miradi maalum inayotekelezwa na wakandarasi wanawake yenye thamani ya zaidi ya shilingi 40,000,000,000.

Mheshimiwa Spika, nitoe pongezi nyingi kwa TANROADS kwa kutenga na kusimamia miradi hii na kwa Katibu Mkuu - Ujenzi ambae kwa miaka mingi amekuwa akisaidia wakandarasi wanawake.

Mheshimiwa Spika, sambamba na hilo sekta ya ujenzi ni sehemu ya sekta binafsi nchini inayochangia 12.5% katika pato la Taifa. Hali ya wakandarasi nchini wanaotekeleza miradi kwa sasa baada ya kupanda kwa bei ya mafuta ni hatarishi dhidi ya ukuaji wa sekta. Serikali itafute fedha za kuwa-compensate wakandarasi kwa mujibu wa conditions of contracts za miradi. Uzuri sekta ilishatabiri hali hizi na kuelezwa vizuri kwenye mikataba.

Mheshimiwa Spika, Waziri atakapo-wind up aeleze mpango na mkakati wa Serikali kuwasaidia wakandarsi wa ndani wanaotekeleza miradi inayoendelea ili kuwanusuru dhidi ya kufilisika.