Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Uyui
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. SHAFFIN A. SUMAR: Mheshimiwa Spika, awali ya yote ninampongeza Mheshimiwa Waziri, Mheshimiwa Naibu Waziri, Katibu Mkuu na wataalamu wote Wizarani kwa kazi nzuri mnayoifanya.
Mheshimiwa Spika, nashauri tuongeze kidogo tozo kwenye mafuta, lakini pia tozo ambazo zimekuwepo zipatikane kwa wakati. Kuna utaalam mpya na wenye gharama nafuu unatumika South Africa ambao tukiutumia itasaidia sana kuziba mashimo barabarani kwa gharama nafuu. Wizara ifanye juhudi za kuujua na kuujaribisha katika barabara zetu.
Mheshimiwa Spika, tuombe mkopo wenye gharama nafuu kutoka kwa African Development Bank mahsusi kwa ajili ya barabara zetu na kiwango cha lami kiwe na maisha zaidi ya miaka 15.
Mheshimiwa Spika, ninaomba sana kuna ahadi ya Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwamba Wilaya ya Uyui barabara iliyopo chini ya TARURA kutoka Magiri kupitia Nsimbo kufika Kigwa kilometa 27 itapandishwa hadhi kuwa chini ya TANROADS na kujengwa kwa kiwango cha lami. Ninaomba sana tulinde heshima ya Rais.
Mheshimiwa Spika, jimbo langu la Uyui, Tabora limepata stesheni ya SGR kwenye Kata ya Nzubuka, ninaomba Wizara ipandishe hadhi barabara ya kutoka Nzubuka kuja Tabora Mjini na ijengwe kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Spika, ninaomba barabara ya kutoka Tabora Mjini – Mambali - Bukumbi mpaka Kahama iko chini ya TANROADS naomba itengewe bajeti ya kujengwa kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Spika, ninaomba barabara ya kutoka Tabora Mjini kuelekea Ulyankulu ina muda mrefu inaahidiwa lami, lakini haijawahi kutengewa bajeti hata mwaka huu wa fedha haijapangiwa bajeti, naomba nisaidiwe maana wananchi waliiamini CCM kwa ahadi hizi.
Mheshimiwa Spika, kuna ahadi ya Rais wetu ya mwaka 2020 alipokuwa Mgombea Mwenza kwamba barabara ya kutoka Mwigelezi mpaka Mabama Centre kilometa tatu ambayo iko chini ya TARURA itajengwa kwa lami, lakini kwa kuwa TARURA haina bajeti ya kutosha, naomba Wizara ichukue hiyo dhamana ya kukamilisha ahadi ya Rais wetu kabla ya mwaka 2030 ili asibakie na deni ambalo litampatia doa mpendwa Rais wetu.
Mheshimiwa Spika, ninaunga mkono hoja na naomba kuwasilisha.