Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027

Hon. Beng’i Mazana Issa

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027

MHE. BENG’I M. ISSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Ninapenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema. Vilevile, ninamshukuru Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake kubwa kwenye sekta hii ya ujenzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kuchangia Bajeti ya Wizara ya Ujenzi ya mwaka 2026/2027 kwenye maeneo ya miradi ambayo sekta hii ndiyo ambayo inasimamia miradi na vilevile inasimamia wakandarasi. Katika miradi mingi ambayo tukitembelea tunavyoona, kwenye kui-design ile miradi kumekuwa na tatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, unakuta miradi inakuwa haifanyiwi feasibility study vizuri na kwa hivyo ninafikiri ni vizuri tuishauri Wizara iweze kuliangalia eneo hili kwa sababu kutofanya feasibility study vizuri kumesababisha kuwa na variations. Yaani zile bei ambazo zimekubalika kwenye mikataba zinabadilika kutokana na hali hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa maana hiyo inasababisha miradi inakuwa ya gharama zaidi kuliko ambavyo Serikali ilikuwa imejipanga kabla ya hapo. Kwa hiyo, ni eneo ambalo linatakiwa liangaliwe sana kwa sababu katika kila mradi, unakuta kuna mapungufu hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ni eneo la uratibu. Unakuta barabara inajengwa kwa mfano, katika barabara ile pia litapita labda bomba la maji na vilevile labda itapita njia ya umeme au itapita njia ya simu lakini unakuta barabara inajengwa mpaka inamalizika, hakuna uratibu ambao unafanyika kati ya hizi sekta ambazo zinakuja kuweka hii miundombinu. Baadaye inasababisha barabara ile either ikatwe ili kusudi miundombinu iweze kutokea. Kwa hiyo kwa sababu Serikali ni moja, tunashauri kwamba uratibu wakati tunataka kutekeleza hii miradi uwepo katika sekta mbalimbali ili kuondoa adha ya vitu kama hivi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo ninapenda kulizungumzia, ni eneo la usimamizi wa mikataba kwa ujumla katika utekelezaji wa miradi. Wakandarasi wengi au kwa kushirikiana na wafanyakazi wa Serikali unakuta usimamizi umekuwa siyo mzuri kuanzia mambo ya uratibu kama nilivyosema, lakini vilevile kuisimamia hii mikataba vile ambavyo inataka. Kwa mfano mikataba yote inakuwa na Bills of Quantities.

Mheshimiwa Mwenyekiti, imezungumzwa hapa Waheshimiwa Wabunge sana tangu asubuhi kwamba thamani au tuseme value ya ule mradi inaweza isifanane. Kwamba unakuta barabara inajengwa lakini haifanani na Bills of Quantities ilivyokuwa inataka. Kwa maana hiyo inaharibika haraka tofauti na vile ambavyo ilikuwa imekadiriwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho ambalo ninapenda kulizungumzia ni wakandarasi. Sekta hii pia inasimamia wakandarasi na kuna Bodi za Wakandarasi na kuna bodi zaidi ya tatu ambazo zinasimamia masuala ya ukandarasi. Tatizo kubwa ambalo limekuwepo kwa wakandarasi wetu wa Kitanzania, kwanza ni nidhamu ya kufanya kazi, lakini pili hawana mitaji. Wengi wao wamekuwa hawana mitaji na hili limekuwa ni tatizo kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kwamba benki zimetengeneza bidhaa za kukopesha wakandarasi ili waweze kupata, lakini wanakuwa saa nyingine hawana vigezo kwa sababu hiyo hiyo ya kukosa mitaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninafahamu kabisa kwamba katika Wizara hii kuna Mfuko wa kusaidia wakandarasi ambao unaitwa Contractor’s Assistance Fund ambao ni Mfuko wa Dhamana. Anatakiwa mkandarasi aombe, halafu benki itamdhamini kwa kupitia Mfuko huo, lakini Mfuko huu una mtaji kidogo. Mtaji wake ni mdogo sana na kwa sababu sisi kama Serikali tumekuja na program ya local content kwamba tuwape wazawa miradi mingi watekeleze wao, ni lazima pia tuwawezeshe. Miradi mingi ya wazawa ina thamani ndogo kwa sababu ya kukosa mitaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa maana hiyo ni kwamba Mfuko uboreshwe ili wakandarasi wetu waweze kupata miradi mikubwa yenye thamani kubwa kama ambavyo wanapata wakandarasi wa nje. Kwa sababu ukifanya kwa assessment ya haraka haraka, kwenye zabuni zinazotolewa hapa nchini, 20% zinakwenda kwa wazabuni wa nje na 80% zinakwenda kwa wazabuni wa ndani, lakini 80% ya kazi thamani yake ni ndogo sana kulinganisha na ile 20% iliyokwenda kwa wazabuni wa nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, yote hii inatokana kwanza ni kukosa mitaji na vilevile kukosa ujuzi na ujuzi hauwezi kupatikana kama hawapewi nafasi ya kupata uzoefu kwenye maeneo hayo. Kwa hiyo ninapendekeza Wizara iangalie jinsi ya kuboresha Mfuko wa Wakandarasi ili waweze kupata mitaji kupitia mfuko wao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho kabisa ni suala ambalo ni la kimkataba. Mikataba mingi sana sasa hivi ya wakandarasi inasema wakandarasi watalipwa advance payment. Advance payment hii imekuwa ni tatizo na ninaona kama imekuwa ni kichaka kwamba kazi haiwezi kuanza bila mkandarasi kulipwa advance payment.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa unakuta kazi hazianzi kwa sababu labda mkandarasi hana fedha kabisa. Kwa nini mkandarasi alipwe advance payment? Lazima tuiangalie hii sheria. Sheria za zamani zilikuwa kwamba kama unaomba kazi, lazima uwe na uwezo angalau wa kukopeshwa ili uweze ku-mobilize kazi yako kwa sababu mobilization ya kazi mara nyingine wala haihitaji hiyo advance payment. Kwa hiyo tuliangalie hili eneo kwa sababu miradi mingi sana ina-suffer kwa sababu ya advance payment.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Muda wako umekwisha Mheshimiwa.

MHE. BENG’I M. ISSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana na ninaunga mkono hoja. (Makofi)