Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busega
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. SIMON S. LUSENGEKILE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipa nafasi nichangie hotuba ya Waziri wa Ujenzi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunazo barabara ambazo zina mashimo makubwa sana. Tunayo Barabara inayotoka Nyanguge – Lamadi na kutoka Lamadi – Maswa. Barabara hii ya Nyanguge – Lamadi imeharibika. Kama ni depreciation zilishakataana. Ninatamani hata kuomba vitabu vya TANROADS ili nianze kuangalia kama hii barabara bado iko kwenye vitabu vyao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika barabara iliyoharibika yenye mashimo makubwa makubwa ni pamoja na Barabara ya kutoka Nyanguge – Lamadi. Ukipita barabara hii ni option yako tu ya kufanya, unatamani kuingia kwenye shimo kubwa au shimo dogo, kwa sababu barabara yote imejaa mashimo. Yanatofautiana tu aina ya mashimo. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lazima tuchukulie serious barabara hii iliyojaa mashimo kutoka pale Nyanguge – Lamadi. Imefikia sehemu hata huyu Mheshimiwa Mbunge Ntemi alipokuwa anazungumza hapa kwamba alitaka kupata ajali ni kwenye hiyo barabara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lazima Mheshimiwa Waziri aje na commitment wakati anakuja kuhitimisha hoja yake. Nimeona kwenye randama yake, ameweka shilingi bilioni 2.5 kwa ajili ya maandalizi ya ukarabati. Sasa sijaelewa maandalizi ya ukarabati, sijui ndiyo anataka kuandika proposal? Yaani mimi sijaelewa hapo maandalizi tunataka kufanya ni yapi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara hii ni lazima iingie kwenye mpango kwa sababu ni barabara ya kiuchumi. Ni barabara inayokufikisha Mwanza, ni barabara inayokupeleka Mara, ni barabara inayokupeleka Simiyu, ni barabara inayokupeleka Geita. Ni lazima tuichukulie maanani ili barabara hii iweze kutengenezwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme jambo moja. Ilipofika hali ya barabara hii waendesha magari, nikiwemo mimi, tunatamani hata kupita njia ya rough road kuliko kupita kwenye ile lami ya kutoka Nyanguge – Lamadi kwa sababu imejaa mashimo. Ukipita barabara ile kwa sasa hivi uwe tu na bajeti ya kupasua tairi mbili wakati wowote. Pamoja na kupasua tairi muda wowote watu pia wanapata ajali kupitia barabara hizi ambazo sasa zina mashimo makubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi tumepita hapa na Mheshimiwa Kiswaga, Mbunge wa Magu, mbele tu ya wapi hapa kabla ya kufika Manyoni, lori moja limeingia kwenye shimo limekita, tairi limepasuka, likaenda kulia likagonga gari, watu watatu wakafa. Hapo tu Manyoni, hata kabla hujafika Manyoni. Kwa nini, kwa sababu ya shimo. Sasa wale waliokuwa na lile lori lililopata ajali na sisi tukakita, tukapasua tairi mbili tukaanza kupeana pole. Ni lazima tuyaangalie mashimo makubwa ambayo yanasababisha ajali kwa Watanzania. Nilitaka kusema hili ili tuone namna ya kuitengeneza Barabara ya kutoka Nyanguge – Lamadi iliyojaa matatizo makubwa kwenye barabara ile. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunalo tatizo kubwa la quality ya barabara. Barabara zinazotengenezwa sasa hivi hazikidhi viwango vinavyotakiwa. Nimekuwa nikifikiria, hivi huyu mkandarasi aliyejenga Barabara ya kutoka Igoma – Nyanguge mbona alijenga kiwango kikubwa ambacho sijui hata ile barabara itaharibika lini? Huyu aliyejenga Barabara ya kutoka Maswa – Lamadi kwa nini hakutujengea vile?
MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Taarifa.
TAARIFA
MWENYEKITI: Mheshimiwa Songe, kuna Taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Emmanuel Cherehani.
MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampa taarifa Mheshimiwa Mbunge, kwamba hata ile barabara inayotoka Manyoni inayokwenda mpaka Tabora, barabara mpya haijamaliza miaka mitatu, nayo sasa ina mashimo yamechimbika ambayo ni makubwa na ni hatari zaidi.
MWENYEKITI: Mheshimiwa Simon Songe, unaipokea Taarifa hiyo?
MHE. SIMON S. LUSENGEKILE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaipokea na ile barabara niliipita mwezi Machi. Hii Barabara ya Manyoni – Tabora Mjini ndiyo ilikuwa priority yangu kupita ile barabara lakini kwa sasa hivi ile barabara muda si mrefu ndiyo itakayoongoza kwa ubovu kuliko barabara zote kwa sababu sasa yenyewe inatengeneza matuta pale katikati, inatengeneza tuta linakuwa hivi, inatengeneza inaenda hivi. Sasa tunashindwa kuelewa huyu mkandarasi alijenga akiwa anawajengea Watanzania kweli au alikuwa analipua kazi za wananchi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, wakandarasi kama hawa watafutwe ili waweze kurekebisha barabara zetu. Tumetumia fedha nyingi za Watanzania, tumetumia fedha nyingi za walipakodi, ni lazima quality ya barabara iweze kuwa nzuri. Otherwise kwa sababu mimi siyo engineer aje aniambie kuna aina nyingi za barabara, kuna ya kawaida, kuna ya kati na kuna ngumu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, labda kama watani-convince kwa style hiyo, lakini kama tuna aina moja ya quality ya barabara tunatamani tujengewe barabara za aina kama ya kutoka Igoma kuja pale Nyanguge. Ni barabara ya mfano tunatamani hata Barabara ya kutoka Nyanguge – Lamadi – Bunda ijengwe kwa staili hiyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi sina tatizo na kuunga mkono hoja, ninaunga mkono hoja, lakini Barabara ya kutoka Nyanguge – Lamadi itengenezwe. Ahsante sana. (Makofi)