Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Vijijini
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. MASANJA K. KADOGOSA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru sana kwa kunipa fursa hii. Kwanza, ninaanza kwa kumpongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa ambayo anaifanya katika miundombinu kwa ujumla, siyo kwa barabara tu katika Taifa letu.
Mheshimiwa Naibu Spika, pili, nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri na timu yake kwa ujumla, kwa hotuba nzuri sana ambayo anaonesha mpango wa Wizara katika mambo ambayo kwa kweli Waheshimiwa Wabunge wamekuwa concerned nayo.
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile nimpongeze sana Eng. Besta, engineer wetu wa TANROADS, CEO wetu wa TANROADS kwa kazi nzuri wanayoifanya katika Taifa hili. Vilevile nimpongeze Meneja wetu wa Simiyu, Eng. Mkumbo kwa kazi kubwa anayoifanya.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa Simiyu ni mkoa mpya, una takribani kama miaka 14 hadi sasa hivi, na una square meter za mraba 25 plus. Pia, kwa upande wa barabara kwa sasa hivi TANROADS haina network kubwa sana Simiyu, wana takribani kama kilometa 200 plus. Kwa maana nyingine tunahitaji Mheshimiwa Waziri atusikilize katika hili, kwamba tunahitaji upendeleo kidogo katika mikoa hii mipya ambayo inajaribu kutafuta maendeleo kwa wananchi.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninajua barabara yetu ambayo inaanzia Lamadi – Maswa inaenda mpaka Mwigumbi Mheshimiwa Rais alitufungulia miaka kama miwili iloyopita, barabara ya kutoka Bariadi – Maswa. Tumepata bahati ya kufanyiwa ukarabati barabara yetu ya kutoka Bariadi kwenda Lamadi. Kwa hiyo, kwa hambo hilo tunaishukuru sana Wizara. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ninajua kwamba wanaendelea na study kwa ajili ya barabara ya kutoka Bariadi – Salama – Magu. Tuna imani kwamba hii stadi itaisha kwa sababu imeanza kitambo sasa. Pia barabara nyingine ya kutoka Nyashimo – Gasamo – Dutwa ambayo inaenda kwenye Jimbo la Bariadi Vijijini, na hiyo tunawashukuru sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna barabara ambayo inazungumza na Waheshimiwa Wabunge wengi sana ya kutoka Karatu – Imbutu – Haydom – Sibiti – Meatu – Lalago inaenda Maswa. Nyingine inakuja Bariadi inaenda mpaka Mwanza. Barabara hii ni muhimu sana, na ninajua iko katika mipango yao, lakini vilevile iko katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema, Simiyu ni Mkoa mpya kama mikoa mingine, kama Katavi. Kwa hiyo, tunahitaji sana barabara zetu kuimarishwa, na ndiyo maana tunapeleka maombi mengi sana kuhusu kuongeza barabara za TANROADS ndani ya Mkoa wa Simiyu.
Mheshimiwa Naibu Spika, barabara mojawapo ambayo Mheshimiwa Waziri tulishazungumza, ni ile ya mzunguko ya kutokea Somanda inaenda Nkololo, inaenda hadi Matongo then inakuja Igego. Barabara ile ni umuhimu sana kwa sababu tunapakana na Mbuga ya Serengeti, almost stretch ya kilometa 80. Vilevile tuna mapori mawili tengefu Maswa Game Reserve na upande mwingine Kijereshi ambayo tunaihitaji sana kwa ajili ya uwindaji.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa ninataka kuzungumzia mambo ya Kitaifa. TANROADS imeanza Julai, 2000. Ukiangalia kwa namna yoyote ambayo wanaweza wakatumia method ya ujenzi whether ni rigid or flexible pavement, obviously lifespan ya barabara inakuwa kati ya miaka 10 hadi 40, kutegemea na ujenzi ulivyofanyika.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ukiangalia barabara nyingi zimejengwa kati ya mwaka 2000 hadi 2026. Maana yake nini? Katika logic ya kawaida, ni lazima barabara nyingi kati ya 30% hadi 40% zimeshamaliza life circle yake. Maana yake nini? Wanapokuwa wanatengeneza plan kwa ajili ya matengenezo ya barabara, maana yake barabara nyingi zinahitaji ku-overhaul.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni ukweli kwamba, tusipochukua hatua ndani ya miaka miwili au mitatu, tutakuwa kwenye crisis. Kwa sababu ukipita kule, na kwa bahati nzuri Waheshimiwa Wabunge wanapita kule, barabara nyingi nyingi zinalia, zinahitaji maintenance, na nyingine zinahitaji overhaul.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa maana yake ni nini? Tusipochukua hatua, maana yake ni kwamba tutajikuta tunaanza kufanya ujenzi ambao is extremely expensive. Tunahitaji kuunganisha barabara sasa hivi kwa badhi ya mikoa iliyobakia, lakini tunahitaji ku-maintain hizi barabara zilizopo.
Mheshimiwa Naibu Spika, maana yake ni kwamba, tusipoziba, kama unaweka maji kwenye ndoo, na kuna matobo chini, maana yake hatuwezi kufikia hayo malengo. Tunahitaji kuunganisha na mikoa, then twende kwenye wilaya. Kwa hiyo, ninaungana na ripoti yetu iliyotolewa na Mheshimiwa Mwenyekiti wetu, lakini vilevile tunahitaji Wizara kuchukua hatua za haraka.
Mheshimiwa Naibu Spika, mambo mengine ambayo ninataka kushauri, hii fedha ya ring fencing, hii siyo tu kwa barabara; reli, maji, kule tunaihitaji kwa sababu ni sheria. Ujue ring fencing ilitokana na sababu ambazo wakati ule waliziona Waheshimiwa Wabunge, ndipo tukaanzisha hii sheria. Kwa hiyo, tusipotii sheria hizi maana yake ni kwamba tunarudi kule tulikokuwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, Mheshimiwa Waziri amezungumzia kuhusu alternative financing. Unapozungumzia bond, ku-issue, ni lazima kuwepo na base ya asset, na ndiyo maana ni muhimu sana kuifanya TANROADS kuwa Mamlaka ili iwe na base hata ya ku-issue bond. Otherwise sijui kama Wizara wanaweza waka-come up hata na guarantee ya Serikali kwa ajili ya ku-issue hizo bond.
Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho ambalo ninataka kuzungumza…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa, muda wako umeisha.
MHE. MASANJA K. KADOGOSA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nimalizie.
NAIBU SPIKA: Malizia sekunde 30.
MHE. MASANJA K. KADOGOSA: Mheshimiwa Naibu Spika, wakati tunazijenga barabara, hali ya reli haikuwa nzuri, lakini sasa hivi tunapoenda, baada ya miaka mitatu, mitano inayokuja, reli itakuwa na hali nzuri. Ni lazima wakae na Mheshimiwa Waziri wa Uchukuzi na yeye wakubaliane mizigo gani inaenda kwenye reli, nao watakuwa wamesha-establish trend mpaka sasa hivi ni mizigo ipi inatuharibia barabara zetu? Mizigo hiyo iende kwa reli, aidha kwa sera au kwa sheria. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuzungumza hayo, ninaomba kuunga mkono hoja, ahsante sana. (Makofi)