Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tumbatu
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachukua fursa hii kukushukuru wewe kwa kunipatia nafasi hii ya kutoa mchango wangu katika Bunge lako Tukufu wa kuchangia katika Wizara hii. Wizara hii ni miongoni mwa Wizara muhimu sana katika nchi yetu, ni Wizara tegemezi katika uchumi wa nchi na watu wake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachukua fursa hii kwa dhati ya moyo wangu kmpongeza Rais wetu, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hasan kwa namna anavyoiongoza nchi yetu kwa umakini mkubwa na kuleta maendeleo makubwa katika nchi yetu. Ninamwomba Mungu ampe afya njema na maisha marefu yenye manufaa naye. Aidha, ampe wepesi wa kazi zake.