Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bumbuli
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. ENG. RAMADHANI H. SINGANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu aliyenipa wasaa wa kuchangia katika Wizara hii ya Mifugo na Uvuvi kwa maandishi. Kwa dhati ya moyo wangu nimpongeze Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Mama yetu kipenzi Dkt. Samia Suluhu Hassani. Kwa mapenzi makubwa na kwa niaba ya Wanabumbuli ninaipongeza Wizara ya Mifugo na Uvuvi; hasa Mheshimiwa Waziri Balozi Dkt. Bashiru Ali Kakurwa pamoja na Naibu Waziri wake Mhe. Ng”wansi Kamani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninawapongeza pia watumishi wote wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuanzia Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu pamoja na watumishi wote walio chini yao. Pongezi hizi kwa Wizara ni kwa sababu ya maandalizi makini ya bajeti yenye dira, iliyoandaliwa kwa weledi na inayoakisi mahitaji halisi ya kila Mtanzania katika maeneo mengi nchini na kwa maendeleo endelevu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mchango wa Jumla (Kitaifa); kuhusu Maendeleo ya Sekta ya Mifugo na Uvuvi; Sekta ya mifugo na uvuvi nchini Tanzania zina mchango mkubwa katika ajira, usalama wa chakula, pato la Taifa, biashara na maendeleo ya viwanda. Licha ya kuwa na mifugo mingi, maziwa makubwa, mito, bahari na mazingira mazuri ya ufugaji na uvuvi, bado sekta hizi zinakabiliwa na changamoto nyingi kama:-
(i) Ufugaji wa kienyeji usio na tija;
(ii) Magonjwa ya mifugo;
(iii) Uhaba wa malisho;
(iv) Uvuvi haramu;
(v) Miundombinu hafifu;
(vi) Teknolojia duni; na
(vii) Ukosefu wa viwanda vya kuongeza thamani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwelekeo wa Kimkakati kwa Tanzania. Tanzania inapaswa kuelekea kwenye:
(i) Ufugaji wa kisasa;
(ii) Uvuvi wa kisasa;
(iii) Uchumi wa buluu (blue economy);
(iv) Viwanda vya kuongeza thamani;
(v) Matumizi ya teknolojia; na
(vi) Uwekezaji katika masoko na Miundombinu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mapendekezo Muhimu ya Kitaifa; kwanza; kuboresha ufugaji; kuanzisha ranchi za kisasa; kuboresha mifugo; kuongeza huduma za chanjo; na kuanzisha benki za malisho.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, kukuza uvuvi wa kisasa kwa kudhibiti uvuvi haramu; kujenga bandari za kisasa za uvuvi; kuanzisha fish farms; na kuongeza vifaa vya kisasa vya uvuvi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu, kuongeza viwanda; viwanda vya nyama, maziwa, ngozi, samaki na chakula cha mifugo;
Mheshimiwa Mwenyekiti, nne, kuimarisha Miundombinu na Masoko; barabara za vijijini; cold storage; masoko ya kisasa; na mifumo ya kidigitali ya biashara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tano, Vijana na Wanawake, kuwapa mikopo na mafunzo kwa vikundi vya uzalishaji, ubunifu wa kilimo na mifugo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, matokeo yanayotarajiwa ikiwa mapendekezo haya yatafanyiwa kazi: Uzalishaji utaongezeka, ajira zitapanuka, mapato ya wananchi yataongezeka, Tanzania itakuwa kitovu cha biashara ya mifugo na samaki Afrika Mashariki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango mahususi kwa Jimbo la Bumbuli kuhusu Maendeleo ya Mifugo; Uvuvi na Uchumi wa Kijamii. Jimbo la Bumbuli lina uwezo mkubwa wa kuwa kitovu cha ufugaji wa kisasa; kilimo cha bustani; ufugaji wa samaki; nyuki na utalii wa mazingira.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo lina Hali nzuri ya hewa, yenye rutuba, maji ya kutosha, mazingira mazuri ya milimani, nguvu kazi ya vijana. Changamoto kubwa za Bumbuli ni Barabara duni vijijini, ukosefu wa masoko ya uhakika, mitaji midogo kwa vijana, teknolojia duni za uzalishaji, ukosefu wa viwanda vya kuongeza thamani, huduma chache za mifugo na uvuvi. Mwelekeo wa Maendeleo ya Jimbo, Jimbo linapaswa kuelekeza nguvu kwenye; maziwa, kuku, mbuzi, ufugaji wa samaki, matunda, mboga, asali na viwanda vidogo vya usindikaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, maeneo muhimu ya kukuza uchumi katika Jimbo:-
(1) Milingano; ufugaji wa ng’ombe wa maziwa na nyama; kuku wa kisasa; kiwanda cha nyama; fish ponds; mnada wa kimkakati wa mifugo na majosho ya kisasa.
(2) Mahenzanguu; ufugaji mchanganyiko Mashamba ya mazao ya mifugo na kiwanda cha nyama.
(3) Soni; Kiwanda kikubwa cha kukusanya maziwa maeneo yote kwa kuwa ndio lango kuu la Halmashari ya Bumbuli na pia karibu na barabara kuu Machinjio ya viwango vya kuweza kukusanya mazao ya nyama kutoka maeneo ya Jimbo la Lushoto na Mlalo.
(4) Baga; ufugaji wa mbuzi, nyuki, matunda. Maboresho ya mnada na Majosho yaliyopo.
(5) Kwemkomole Fish ponds, Poultry projects na ufugaji wa mbuzi wa kisasa.
(6) Nkongoi; kilimo cha mboga, maziwa, umwagiliaji kwa ajili ya mazao ya mifugo.
(7) Bumbuli na Dule B; fish ponds, ufugaji wa maziwa na kiwanda cha maziwa.
(8) Mayo na Kisiwani; utalii, trout farming na kilimo cha matunda.
(9) Usambara; Eco-tourism na Organic farming.
(10) Vuga; Mafunzo, viwanda vya chakula vya mifugo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mapendekezo ya Jumla kwa Bumbuli ni kama ifuatavyo:-
(i) Kuboresha barabara za vijijini;
(ii) Kujenga masoko ya kisasa;
(iii) Kuanzisha cold rooms;
(iv) Kuwezesha vijana na wanawake;
(v) Kuimarisha vyama vya ushirika,
(vi) Kuanzisha viwanda vidogo vya maziwa; Asali; Nyama na matunda;
(vii) Kutumia teknolojia za kisasa za uzalishaji; na
(viii) masoko.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hitimisho; kwa uwekezaji mzuri na mipango ya kimkakati, Bumbuli inaweza kuwa Kitovu cha kilimo cha milimani; Mfano wa ufugaji wa kisasa; Eneo la utalii wa mazingira; na Chanzo kikubwa cha ajira kwa vijana na wanawake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, maendeleo ya jimbo yatategemea; Miundombinu bora; Elimu na mafunzo; Ushirikiano wa wananchi; na Uwekezaji wa muda mrefu katika sekta za uzalishaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha.