Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. CHIKU A. ISSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nianze kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa juhudi zake kwa kuhakikisha Wizara ya Mifugo na Uvuvi inapata fedha za kutosha na kuwawezesha kusambaza vifaa muhimu katika maziwa yetu yote. Nimpongeze pia Waziri, Mheshimiwa Bashiru Kakurwa na Naibu wake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nishauri kufanyike utafiti kwa nini kuna uvuvi haramu kwa wakati huu kitu ambacho kwa miongo ya nyuma haukuwepo, kudhibiti nyavu zisizofaa ili kuondoa kiini cha tatizo ulinzi uongezwe kutumia vifaa vya kisasa vya kidijitali kubaini wavuvi haramu, niombe kutoa ushauri kwa Mkoa wa Arusha. Tunaomba Serikali ije na mkakati thabiti wa kujenga mabwawa ya maji ya kunyweshea ng'ombe na mifugo mengine, katika maeneo ya Wilaya ya Monduli, Longido, Ngorongoro yanakuwa na hali mbaya sana wakati wa kipindi cha ukame (kuvuna maji mengi tunayoyapata wakazi wa mvua za masika)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba Wizara ije na mpango mkakati wa kuanzisha ufugaji wa samaki katika ukanda huu na hii kupitia vikundi vya akina mama na vijana wapate ujuzi kupitia wataalam kutoka wizarani, hii itatusaidia kuongeza ajira, kukuza uchumi wa mkoa wetu. Tuanze kwa haraka uzalishaji wa majani kwa ajili ya malisho ya mifugo kuunda idara itakayoshughulikia na kupanua masoko ya mifugo na ngozi ya mifugo yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninawapongeza Waziri, Naibu Waziri na Watendaji wote katika Wizara wa Mifugo na Uvuvi. Ninaunga hoja mkono kwa kesho iliyo bora.