Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027

Hon. Kinjikitile Ngombale Mwiru

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kaskazini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027

MHE. KINJEKITILE N. MWIRU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa nafasi hii. Kwa kuwa leo ni mara yangu ya kwanza kuongea katika Bunge hili, ningependa sana kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunifikisha hapa, pia ningependa kukishukuru Chama changu Cha Mapinduzi kwa kuniamini na kunipa nafasi ya kuongoza wananchi wa Kilwa. Shukrani za dhati na za kipekee, ninapenda kumshukuru Mwenyekiti wa Chama Changu Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na mwisho ningependa kuwashukuru wananchi wa Jimbo langu la Kilwa Kaskazini pamoja na familia yangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeifuatilia hotuba ya Waziri, ninapenda kumpongeza kwa hotuba nzuri aliyowasilisha leo Bungeni. Ninaomba nichangie hoja zangu, kwanza kabisa ninapenda nimshukuru tena Rais wangu Dkt. Samia Suluhu kwa kutujengea bandari kubwa ya uvuvi ya kisasa katika Wilaya yetu ya Kilwa Kaskazini, Mkoa wa Lindi, tunamshukuru sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nielekeze mchango wangu kwenye mambo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ni migogoro ya wafugaji na wakulima. Ninatokea katika Jimbo la Kilwa Kaskazini ambalo asili yetu ni uvuvi na ukulima, lakini hivi karibuni shughuli za mifugo zimeongezeka sana ambazo zimekuwa zikituletea matatizo mengi sana kati ya wananchi na wafugaji, ambayo yametusababishia madhara mengi sana na kuhatarisha usalama wa wananchi, kusababisha vifo, majeruhi na kupoteza mali. Hivyo tunaiomba Serikali kulichukulia jambo hili kwa uzito wa kipekee kukomesha kabisa matatizo haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili na la mwisho ni shughuli za uvuvi. Wilaya yetu ya Kilwa ina fukwe za takribani kilomita 170 ambazo wananchi wanashughulika na shughuli za uvuvi, ninaomba Mheshimiwa Waziri atuangalie kipekee katika mgao wako wa maboti sisi wananchi wa Jimbo la Kilwa, kwa sababu uvuvi ndiyo uti wa mgongo wa wakazi wa Kilwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na ninaunga mkono hoja. (Makofi)