Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalambo
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. EDIFONSI J. KANONI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa kunipa nafasi ili nichangie Bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa nafasi, lakini kipekee nimshukuru Mheshimiwa Rais kwa kumwamini Mheshimiwa Dkt. Bashiru Ally kwa kumpa nafasi ya kuwa msimamizi wa Wizara hii ya Mifugo na Uvuvi. Pia, niwashukuru sana watendaji wake wote ambao wanampa ushirikiano kutimiza majukumu yake. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitakuwa na machache, kwanza kuishukuru Serikali kwa jinsi ambavyo Mheshimiwa Rais ameendelea kutujali katika maeneo ya Ziwa Tanganyika. Tumepokea pia boti kwa ajili ya doria na tumeendelea kupokea mikopo kwa ajili ya wavuvi; hiyo yote tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Wavuvi wa Ziwa Tanganyika na maeneo mengine hali ya Ziwa Tanganyika ni mbaya sana. Hali ya Ziwa Tanganyika ni mbaya sana, mazingira ya uvuvi ni mabaya; kuna uharibifu mkubwa sana wa mazingira, kadhalika ninafikiri hata Ziwa Victoria, hali ni mbaya kwa sababu uvuvi haramu bado upo na umeshamiri sana, samaki wameadimika hawapatikani. Nimwombe sana Mheshimiwa Waziri kuendelea kusimamia sheria na miongozo waliyonayo kuhakikisha kwamba wananusuru Ziwa Tanganyika na Ziwa Victoria, hali ni mbaya sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, pia Ziwa Tanganyika tunapakana na nchi nne; Tanzania tunamiliki 41%, Kongo 45%, Burundi asilimia nane na Zambia asilimia nne. Hili eneo lina wakazi wanaotegemea uvuvi karibu katika Ziwa Tanganyika wanaozunguka hili eneo ni karibu 10,000,000.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba sana kwa heshima kubwa kwa kuwa ninaamini kabisa utendaji wako wa kazi siyo wa mashaka mashaka; kuongeza nguvu katika kudhibiti uvuvi haramu. Uvuvi haramu umeshamiri sana, pia kumekuwa na doria ambazo wamekuwa wanafanya operation kwa ajili ya kudhibiti uvuvi haramu wanaoathirika ni wavuvi wadogo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niishauri Serikali wadhibiti kwanza wale wanaosambaza, kwa sababu wavuvi hawa shida yao ni kujikimu; kwa hiyo, hawawezi kuacha kutumia nyavu haramu, lakini nyavu haramu zinapatikana wapi? Zinapatikana kwenye maeneo yetu, siyo kwamba Serikali haiwajui wanaosambaza hizi nyavu haramu. Kwa hiyo, kuliko kwenda kumbuguzi mvuvi ni bora wakadhibiti uvuvi haramu na wale wanaosambaza ili kukomesha kabisa, kwa sababu mbona zinapatikana? Kama zinapita mpaka zinaenda kufika kwa wavuvi kule na wakati wanafanya doria wanakwenda kuwakamata. Lakini wavuvi wameendelea kuathirika sana katika doria wanazozifanya ikiwa ni pamoja na kuwakamata, kuwapiga faini, kuwafunga, lakini kuwafilisi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, nishauri tena kuhakikisha kwamba wanadhibiti hawa watu wanaochukua hizo nyavu au vifaa hivyo haramu ili kuhakikisha kwamba wanakomesha kabisa. Hata hivyo, wamekuwa wakifanya doria, sioni sehemu ambayo kwa maeneo yetu kama Ziwa Tanganyika kutoka Kigoma, Katavi pamoja na Rukwa, wanateketeza hizo nyavu baada ya kukamatwa. Kwa maana hiyo, zikishakamatwa, zinarudi tena kwenda kufanya uhalifu. Sasa ni shughuli ambazo unaweza ukakuta kuna watu wamejiwekeza huko kwa ajili ya kujipatia kipato haramu. Ninaomba Mheshimiwa Waziri atusaidie kudhibiti uvuvi haramu ili kuweza kunusuru.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hali ya wavuvi katika Ziwa Tanganyika ni mbaya sana, ni mbaya sana kwa maana wanavua hawapati samaki kutokana na uharibifu wa mazingira. Hata hivyo, nimwombe Mheshimiwa Waziri, kumekuwa na mpango wa kupumzisha hili Ziwa Tanganyika, lakini hili ziwa kutokana na jinsi ambavyo tunaligawa katika nchi nne, kuna maeneo wanafunga na maeneo mengine hawafungi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwombe Mheshimiwa Waziri kwa heshima kubwa, katika mwaka huu, wakati wanaendelea kufanya tathmini katika vipindi ambavyo huwa wanafunga kwa miezi mitatu, wawaachie wananchi wasifunge hili ziwa kwa mwaka huu. Kwa sababu hata katika miaka hii miwili, mitatu hali ya uvuvi Ziwa Tanganyika ni mbaya, kwa hiyo, hata wakiendelea kufunga lile ziwa linajifunga na kujifungua.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la msingi ninaloweza kushauri ni kudhibiti uvuvi haramu ili tuwe na uvuvi endelevu. Kuna nyavu wanazotumia na Mheshimiwa Waziri anajua, ambazo zikikatika ndani ya maji zinaoza baada ya miaka 100 kwa tathmini ambavyo wataalam wamesema. Sasa tukiacha uvuvi haramu ikiendelea ndani ya miaka hiyo 50 au miaka 20 tutabaki na maji matupu hatutakuwa na samaki tena. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwombe sana Mheshimiwa Waziri ziwa lisifungwe, watoe elimu. Nimshauri pia aunde makundi katika maeneo ya kata na vijiji, ukanda wa maziwa kwa kuanzia Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika. Walinzi wa Ziwa Tanganyika wawe wavuvi wenyewe, wataalam wanakuja baadhi ya watumishi ambao ni Sekta ya Uvuvi siyo waaminifu wana mtandao mkubwa. Bila shaka Mheshimiwa Waziri anajua kwamba, kuna mtandao mkubwa kuanzia ngazi ya kata kwa watumishi, siyo wote lakini baadhi wana mtandao ambao wanashirikiana na hawa ambao wanafanya shughuli za uvuvi haramu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine, upande wa wafugaji, katika Jimbo lilotoka la Kalambo, Mkoa wa Rukwa tumeendelea kupokea ndugu zetu hawa wafugaji kutoka kanda ya ziwa na maeneo mengine. Hawa ni wawekezaji kama wawekezaji wengine tunawapokea kwa mikono miwili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwombe Mheshimiwa Waziri, hawa ndugu zetu kumekuwa na changamoto kati ya wafugaji na wakulima; niombe elimu iendelee kutolewa kwa sababu maziwa tunahitaji na nyama tunahitaji, kwa hiyo, mahusiano yawe ni kipaumbele. Hawa wafugaji wanapokuja kuna muda wanatumia nguvu kubwa sana kwa wenyeji ambao ndiyo wamewapokea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kuna uwezekano Wizara hizi za Kisekta kama Ardhi, kuwe na utaratibu kwa sababu migogoro mingi inaanzishwa na baadhi ya viongozi wa vijiji kwa kuuza maeneo kwa hawa wageni bila kufuata taratibu mwishoni inakuwa ni migogoro mikubwa. Ili kama kuna uwezekano tuangalie Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji mwisho wake wa kuuza ardhi ni kiasi gani? Sasa Mwenyekiti wa Ardhi anaenda kusaini mkataba wa hekari 1,000, anakuwa sheria hazijui na baadaye inaleta shida.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wadhibiti pia leseni ambazo zinatoka Wizara ya Uvuvi, zinafanya export nje, ambazo zimeendelea kukodishwa bila kufuata taratibu na mwisho kuharibu soko la samaki katikati ya Tanganyika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo ninakushukuru sana na ninaunga mkono hoja kwa asilimia mia moja. (Makofi)