Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Vijijini
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. MASANJA K. KADOGOSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa fursa ya kuchangia, lakini vilevile ninampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa ambayo anaifanya kwa wafugaji. Mnajua katika kampeni ufugaji ilikuwa ni ajenda moja kubwa sana, ambayo ameizungumzia kwa upana, lakini hata kwenye Ilani yetu ya Chama cha Mapinduzi, kwa miaka mitano inayokuja inasema kwamba, wataongeza malisho kutoka ekari milioni 3.4 mpaka milioni sit ana vilevile, itakuwa imetoa ruzuku kwenye chanjo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, bahati nzuri sisi watu wa Bariadi huko tumebahatika kuwa katika ufunguzi wa chanjo, ulifanyikia Bariadi. Kwa hiyo, kuna juhudi kubwa sana imefanyika. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile katika hali ya kutengeneza miundobinu ya wafugaji kwetu, kwa Bariadi vijijini kuna ujenzi wa mabwawa kule na kuna majosho. Kwa hiyo, unaweza ukaona juhudi na mtazamo wa Serikali kuona kwamba, wafugaji kuna transformation kubwa. Nina-declare interest, vilevile mimi ni mfugaji wa Samaki. Kwa hiyo, ni area ambayo kidogo ninaweza nikaizungumzia kwa ufasaha kwa sababu, nimo ndani humo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile ninampongeza sana Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziri, wanafanya kazi nzuri sana kwa kweli, mara nyingi unakuta hawakai. Set up ya Wizara hii kwa kweli, Mheshimiwa Dkt. Bashiru tukimwona amekaa tutakuwa na mashaka sana kwa sababu, ni Wizara ya kutembea. Pia, ninamshukuru na kumpongeza Mwenyekiti wa Kamati kwa taarifa nzuri sana aliyoitoa. Ninaamini imetuongezea maeneo ya kuzungumza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Sekta ya Mifugo ni muhimu sana katika Taifa letu. Ukiangalia dira yetu katika ukurasa wa 58, nitasoma kidogo, zimetajwa sekta zenye fursa ya mageuzi kuelekea 2050. Inasema, “Sekta ya Mifugo itaboresha kwa kuwekeza,” ni muhimu sana ku-underline neno “kuwekeza katika uzalishaji wa kisasa” neno “kisasa”; “...wa bidhaa zinazotokana na mifugo kwa kuongeza tija na thamani, ili kukidhi mahitaji ya masoko ya ndani na nje. Sekta ya Uvuvi itaimarishwa kwa kuendeleza uvuvi na ufugaji wa Samaki”, mwisho wa kunukuu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni obvious kwamba, Sekta ya Mifugo na Uvuvi imewekwa chini ya Sekta ya Kilimo, lakini ni muhimu sana tunapofikiria kwamba, baada ya miaka 25 tuwe na huo uchumi wa one trillion, Sekta ya Mifugo ina contribution kubwa sana. Maana yake nini?
Mheshimiwa Mwenyekiti, maana yake ni kwamba, pamoja na kazi kubwa ambayo mnaifanya sasa hivi ya kuleta mageuzi, tunahitaji transformation kubwa sana kwenye Sekta ya Mifugo. Unapozungumzia mifugo na uvuvi, maana yake ni kwamba unazungumzia ardhi kwa sababu, lazima utafuga kwenye ardhi. Unazungumzia malisho, unazungumzia maji, kwa hiyo, transformation kubwa pamoja na technology; ina-revolve katika hivyo vitu ambavyo tunavitaja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la mindset ambalo tunazungumzia kwa kufanya transformation kutoka kwenye ufugaji ambao tunao sasa hivi kwenda huko tunakokutaka. Sasa, mindset siyo kitu ambacho ni kirahisi na kwa Wizara. Ushauri wangu ni kwamba, wajiwekee muda. Ni muhimu sana wanapokuwa wana-deal na hili jambo wawe na mashamba darasa, kama Mheshimiwa Waziri ulivyozungumza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mashamba darasa haya hatuwezi kuwa wafugaji wote, kuwepo na focus. Mnaweza kuwepo na maeneo ambayo pengine yanastahili sana kwa ufugaji wa ng'ombe wa nyama au kuna sehemu nyingine wanaweza wakastahili, kwa ajili ya maziwa. Isiwe kila sehemu tunafanya hicho hicho. Kuwepo na focus na persistence kwa sababu, hili jambo linahitaji muda kidogo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, nigusie kwenye uvuvi. Kwa sababu ya muda wenyewe ni mdogo, lakini katika uvuvi kitu ambacho ninakiona ni suala la utafiti, kuwa na mbegu bora; na hili ni hata kwenye mifugo. Suala la utafiti ninafikiri bado tunahitaji uwekezaji mkubwa katika upatikanaji wa mbegu. Leo hii mtu anayetaka kufuga samaki kwenye cages zile, ukitaka tuseme labda vifaranga 200,000, Mzee Sariki yuko hapa, Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa zamani; huwezi ukapata lazima uende nchi ya jirani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninajua muda hautoshi, lakini ninaunga mkono hoja. Mengine bahati nzuri Doktor tunazungumza na ni schoolmate Wangu, nitazungumzanaye face by face. Ahsante sana. (Makofi)