Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. SELINA H. KINGALAME: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipatia nafasi, ili niweze kuchangia kwenye bajeti hii ya Katiba na Sheria. Kwa kuwa, ni mara yangu ya kwanza kusimama kwenye Bunge hili Tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninapenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa uzima, afya na kibali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, ninamshukuru sana Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia, ni Mwenyekiti wetu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kunipendekeza, kuteua jina langu na hatimaye leo niko humu kwenye Bunge hili Tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninawashukuru sana vilevile Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa UWT, Taifa kwa kunipa kura nyingi za kishindo. Ninawaahidi ile imani waliyonikopesha, basi nitawalipa kazi na utu. Mwisho, ila siyo kwa umuhimu, ninaishukuru sana familia yangu kwa upendo na kwa kuniombea muda wote, Mwenyezi Mungu awabariki sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba sasa nijielekeze kwenye kuchangia katika bajeti hii ya Katiba na Sheria. Kwanza ninampongeza Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa anayoifanya, lakini pia, ninampongeza Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria, kaka yangu, Mheshimiwa Juma Homera, hongera sana kwa kazi kubwa anayoifanya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, iIle programu ambayo wameianzisha, Wizara ya Katiba na Sheria, inayosema 'Ongea na Waziri', ambayo wananchi wanaongea moja kwa moja na Waziri wa Katiba na Sheria, wanapeleka malalamiko yao, hongera sana kwa programu hiyo. Pili, nampongeza Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, dada yangu, Mheshimiwa Zainab Katimba, hongera sana kwa kumsaidia Mheshimiwa Waziri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaelekeza mchango wangu kwenye jambo moja tu, jambo hilo ni Law School of Tanzania. Law School of Tanzania ilianza mwaka 2007, ni ukweli usiofichika Law School of Tanzania ipo moja tu Dar es Salaam, lakini lengo kuu la kuanzisha Law School of Tanzania ni kutoa mafunzo kwa vitendo kwa wahitimu wa sheria, ili waweze kuwa mawakili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni ukweli usiofichika sasa hivi vyuo vinavyotoa Degree ya Sheria ni vingi, lakini hata wahitimu ambao wanamaliza Degree ya Sheria ni wengi. Kwa mwaka wa fedha 2023/2024 wahitimu waliomaliza Degree ya Sheria karibu 4,373 walimaliza, lakini kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 pia, wanafunzi waliomaliza Degree ya Sheria walikuwa 5,008.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba niishauri Serikali yangu, pamoja na Wizara hii, waone namna ya kuweza kuongeza branches za Law School of Tanzania, ili kupanua wigo wa kuanzisha matawi kwenye mikoa tofauti tofauti. Wanaweza wakaanza hata kwa kanda; wakaanza hata Kanda ya Kati, Kanda ya Ziwa mdogo mdogo, ili kuwatendea haki hawa wasomi wa sheria, ambao nina imani Serikali yangu sikivu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania italiangalia hili suala kwa jicho la tatu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo ninaomba niwapongeze sana Wizara ya Katiba na management yote na ninaomba kuunga mkono hoja. (Makofi)