Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027

Hon. Aziza Sleyum Ally

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027

MHE. AZIZA S. ALLY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia. Nichukue nafasi hii kuipongeza Wizara hii kwa kazi nzuri ambayo wanayoifanya. Sisi Wanakamati wa Kamati yetu ya Katiba na Sheria tunafanya kwa ukaribu zaidi na Wizara yetu hii kwa Waziri, Naibu Waziri, Watendaji na Wakurugenzi wote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kitu cha ajabu tunapofanya hata ziara tunakwenda na Waziri, Naibu Waziri, Wakurugenzi wote na Watendaji mpaka kwa Katibu Ofisi ya Rais tunakuwa nao. Kwa hiyo Kamati yetu na Wizara tunafanya kazi kwa pamoja kwa ushirikiano. Tunaomba Waheshimiwa Wabunge watuamini tunaisimamia na tunasimamia maslahi ya wananchi katika Wizara hii na ni Wizara sikivu na inafanya kazi yake vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kijana wetu Ridhiwani ni Waziri wetu lakini ni Waziri ambaye anayejishusha ana nidhamu ana heshima kwa kila mmoja. Ninachukua nafasi hii nisipolisema hili pamoja na Naibu wake Waziri kwa kweli sitowatendea haki. Ridhiwani ni kijana lakini kazi zake anazisimamia kwa weledi zaidi. Ninampongeza sana mtoto wetu, kijana wetu kwa kazi hiyo, lakini si kwa mara ya kwanza ni muda wote ambao tunafanya kazi anafanya kazi vizuri. Hongera sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nizungumzie kuhusu TASAF. Kipindi kilichopita tulianza kuwa na TASAF One ambayo na imani ilikuwa ni kipindi cha Rais wetu Mkapa, marehemu. TASAF One ilifanya kazi vizuri tulikuwa na Mkurugenzi ambaye alikuwa akiitwa, Dkt. Likwelile naye pia ametangulia mbele ya haki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapongeza tukaingia TASAF II, TASAF III mpaka hivi sasa tumeweza kufika TASAF IV ambayo tuseme ni TASAF IV ambayo mpaka tunafika hapo Serikali yetu imefanya kazi vizuri, usimamizi wa TASAF kwa wananchi ulikuwa ni mzuri, ndiyo maana tumeweza mpaka kufika hii TASAF IV.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaipongeza sana Serikali, ninawapongeza watendaji na kumpongeza pia Mkurugenzi wa TASAF Dkt. Mziray. Hongera kwa kazi kubwa ambayo ameifanya na hatimaye tumefika kwenye TASAF IV, hongera sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashauri kutokana na haya ambayo tuliyaona TASAF III tuliyoifanya Mwanzam ninategemea tukienda kwa utaratibu huo mpaka TASAF IV tutaweza kuwafikia kwenye Wilaya zote kwa kuanzisha vikundi vya akina mama kama vile vilivyoanza vya vijana, hata vya wazee ambavyo vitafanya vizuri sana. Waziri Ridhiwani alikuwepo pale na aliona na alikabidhi vitu vingi pale katika vikundi vile vya akina mama, hongera sana kwa kazi ile iliyofanywa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninategemea TASAF hizo na vikundi hivyo vitaweza kufika mpaka kwenye Wilaya yetu mpaka kufika kwenye Mkoa wa Tabora, akina mama warina asali wengi wananufaika kutokana na TASAF hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba niende haraka, ninaona muda unaenda, niongelee kuhusu ajira kwa vijana. Tunampongeza Rais kwa kutoa kibali vijana wengi kuajiriwa, lakini ninaomba nitoe ushauri kuhusu vijana wanaojitolea, hawa wanajitolea na wanafanya kazi wengine mpaka wanazeeka, lakini kuna mwongozo ambao tunaotegemea uje ili mwongozo huo uweze kuonesha hawa vijana wanaojitolea je, mwongozo utasimama vipi ili tuweze kukamilisha mwongozo huo wa vijana wengi waweze kujitolea na kuweza kupata ajira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba niongelee kuhusu Mradi wa Watumishi House. Mradi huu ni mzuri sana kama tutausimamia vizuri katika wilaya zetu na mikoa yetu. Waziri Ridhiwani huu ni mradi ambao unaweza ukainua kelele za watumishi wote nchini kama tutauongezea fedha, tutaupa nguvu na tutaupa nafasi kubwa ya kuweza kufanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia hutotosha kama utatumia nafasi kubwa ya kuwapa elimu Wabunge wauelewe vizuri mradi huu wa Watumishi House, nadhani hapo ulipo utaondoka na utasogea kwa kiwango kikubwa zaidi, watumishi wengi watapata nyumba za kukaa, kuanzia kwenye wilaya, vijijini na kwenye kata ambako shule zetu zinajengwa na Madaktari tunapiga kelele watapata nyumba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huu ni mradi mzuri na unafanya kazi vizuri, Ofisi ya Rais umefanya kazi vizuri kwa kuweza kuwaletea na kuwajengea uwezo mkubwa watumishi wetu. Tunamwomba Waziri alete utaratibu wa elimu kwa Wabunge wote ambao utaweza kutusaidia sana kuweza kumpigania na kumwombea apate pesa nyingi ili mradi huu uinuke na ufanye kazi vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nichukue nafasi hii kumpongeza Rais katika Wizara yake hii ya Utumishi wa Umma kwa kazi kubwa anayoifanya, anafanya kazi kubwa. Mama huyu muda mwingi utamkuta anafanya kazi, nina imani muda wake wa kutulia ni mchache sana. Anafanya kazi matokeo yanaonekana, ari anayo, nguvu anayo, ujasiri anao, mama yangu afanye kazi, Mwenyezi Mungu ndiyo atamlipa kwa kiasi kikubwa na afya njema Mungu atamjalia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba niunge mkono hoja. (Makofi)