Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu Mwaka wa Fedha 2026/2027

Hon. Kija Limbu Ntemi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Katoro

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu Mwaka wa Fedha 2026/2027

MHE. ENG. KIJA L. NTEMI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana. Nami nipate fursa ya kumshukuru Mwenyezi Mungu aliyetuongoza mpaka kufika wakati huu tukiwa salama salimini kama Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimshukuru na kumpongeza pia Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyenipendekeza mimi kuwa Mbunge wa Jimbo la Katoro, siyo mimi tu na vijana wote waliopendekezwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuingia Bungeni mara ya kwanza, wengine wakachaguliwa kuwa Mawaziri, Naibu Mawaziri kwa mara ya kwanza katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeza vilevile Makamu wa Ras, Dkt. Emmanuel Nchimbi aliyesimama, kumtetea na kumwombea kura Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan naye pia kuwa Makamu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia nimshukuru na kumpongeza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kaka yetu, Ndugu yetu Dkt. Mwigulu Nchemba anayefanya kazi katika sehemu nyingi, amezunguka nasi tumemwona, mambo mengi ameyatatua papo kwa papo ili kuonyesha kwamba Serikali iko pamoja na wananchi wake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Dkt. Mwigulu alisema anakuja Katoro na nikapata taarifa kwamba atafika Katoro, tulijiandaa sana watu wa Katoro kumpokea ili azungumze nasi, atutie moyo, awatie moyo watu wa Samia ila sasa kwa sababu ya ratiba akashindwa kufika. Tunamwomba baada ya Bunge hili Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania afike Katoro ili watu wa Katoro aone wanavyokuzungumza na wanavyomzungumza Rais.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwampongeza pia Spika wa Bunge, Naibu Spika na viongozi wote walioteuliwa na Rais wakiwemo Mawaziri na Naibu Mawaziri wanaofanya kazi vizuri, akiwemo mtu ambaye tumepewa Jimbo kwa pamoja, tukagawiwa tukapewa, kaka yangu Dkt. Jafar, Naibu Waziri TAMISEMI, huyo ni pacha wangu kabisa ambaye tuko naye sehemu moja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungmze kidogo kwa kuwashukuru Chama changu cha CCM, kuanzia Mjumbe aliyenipigia kura mpaka Kamati Kuu walionipendekeza walioko Jimbo la Katoro, walionichagua mimi kuwa Mbunge wa Jimbo la Katoro.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamshukuru nami mke wangu aliyeniombea sana kila siku wakati tunaomba kura, kila siku asubuhi tuliomba tunakwenda kwenye kampeni tukimwombea Rais tunapiga magoti, tukiombea na wagombea wote hata wale ambao tulikuwa tunaomba nao kura, tulikuwa tunawaombea pia afya njema ili tuendelee kufanya kazi kwa pamoja kuomba kura kwa wananchi. Kwa hiyo, ninamshukuru sana mke wangu Mariam aliyenipigania sana kusimama hapa kufika sehemu hii pia. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nizungumze basi machache baada ya shukrani hizo, lakini kama kuna shukrani ambazo nimezisahau ninaomba Mungu atawakumbusha kwa mioyo yao kwamba nimewashukuru pia na wao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikimshukuru Dkt. Samia Suluhu Hassan juzi niliomba gari la zimamoto hapa, Waziri wa Mambo ya Ndani alitamka gari litakuja na Dkt. Samia Suluhu Hassan akanipatia gari la zimamoto leo lipo Katoro, leo hii nikimshukuru Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tena nimeambiwa kiwanja cha kujenga ofisi za zimamoto ndani ya wiki hii kitapatikana usipomshukuru mtu unafanyaje? Ninamshukuru Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa haya mambo anayoendelea kutufanyia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati wa kampeni za Dkt. Samia Suluhu Hassan alisimama Katoro tukamshuhudia tukamwona, wakati anasimama Katoro, barabara za Katoro zilikuwa zinajengwa mitaro na sasa barabara nyingi zinapitika alipoapishwa na barabara zimeanza kupitika, mitaro imejengwa, tunawaomba TARURA watuongezee mitaro ili Rais hata kama siku moja akija Katoro aweze kupita barabara yoyote anayopenda yeye mwenyewe, kwa sababu zitakuwa zimekuwa salama zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninayo barabara moja inaitwa Luhuha ambayo iko chini ya TARURA inayopitisha mazao kutoka katika Kata Sita kuleta Mji wa Katoro, ambazo hizo Kata ni pamoja na Kata ya Butundwe, Kata ya Nyakagomba, Kata ya Chigunga, Kata ya Bukondo, Nyamwilolelwa na Nachiluluma ambazo zilikuwa zinasumbua sana, lakini kwa sababu tunao viongozi wazuri wa TARURA na Meneja wetu wa Wilaya ya TARURA tulizungumza naye amerekebisha zile barabara zinapitika vizuri mpaka sasa tunawapongeza sana TARURA, mnafanya kazi vizuri endeleeni kusimamia kila sehemu ili barabara hizi ziweze kupitika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba TAMISEMI kuna Kata mbili ambazo zinazo changamoto za vituo vya afya, Kata ya Magenge na Kata ya Kaseme, ikiwezekana katika bajeti hii basi wale watu waweze kupatiwa kituo cha afya ili waweze kujiendesha wenyewe, ili waweze kupata huduma ya afya katika mazingira yao na siyo kutoka kule kuja Katoro kwa ajili ya kupata huduma ya hospitali. Ninaamini ninyi ni wasikivu ninaamini tunayo Serikali sikivu itatufanyia haya mambo na baada ya bajeti zao wafike kwenye maeneo yetu ili waweze kufanya kazi hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina Kata tatu au Kata mbili, Kata ya Ludete na Kata ya Katoro yenyewe ambazo ziko mjini zinazohitaji kuunganishiwa sana maji. Rais ameyatoa maji mbali kabisa ambako hata wengine hawapajui panaitwa Chankolongo. Chankolongo ni mbali ametoa maji kwa gharama ya bilioni sita ameyaleta katika Mji wa Katoro, kilichobaki ni usambazaji wa maji na naamini kwa sababu Waziri wa Maji yupo na Naibu wake na tumezungumza nao mara nyingi sana, wamesema wataanza kuyasambaza maji yale yaliyoletwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ili watu wa Katoro waendelee kupata maji safi na salama katika Mji wa Katoro.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, Mbunge wa Jimbo la Katoro ninaunga mkono hoja bajeti ya Waziri Mkuu, ahsante sana. (Makofi)