Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kavuu
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kupata nafasi ya kuwa mchangiaji pekee kwenye Wizara hii ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. (Makofi)
Kwanza kabisa nimshukuru Mheshimiwa Waziri kwa kunipa nafasi ya kuwa mpambe wake leo, lakini kipekee kabisa niishukuru Kamati kwa wasilisho lake na katika mazingira ya kawaida yale yote ambayo yamependekezwa na Kamati yanakwenda kufanyiwa kazi na Wizara ili kuleta ufanisi uliosahihi kabisa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, sikutarajia kuwa mchangiaji pekee, kwa hiyo wakati mwingine unaishiwa hata maneno ya kupangilia habari, lakini ukweli ni kwamba maeneo ambayo Mheshimiwa Waziri ameyawasilisha hapa katika bajeti yake ni maeneo muhimu kabisa kabisa na sisi kama Wabunge lazima tukayafanyie kazi kwa usahihi wa kutosha kabisa kwa sababu ni maeneo ya kiushahuri na chombo hiki kwa umuhimu wake kwa kweli katika baadhi ya maeneo ambayo kimsingi yanatakiwa kuzingatiwa ni yale maeneo ambayo tunakwenda kuyatumia kwa shughuli za jeshi.
Mheshimiwa Spika, nitoe tu ushahuri kwa wananchi katika maeneo haya kimsingi huwa ni maeneo hatarishi kwa sababu matumizi yale ya kijeshi huwa yanabaki yanaacha baadhi ya masalia ya vyombo ambavyo vilitumika huko kama mabomu na nini, kwa hiyo, maeneo yote haya ambayo ni maeneo maalumu kwa ajili ya matumizi ya jeshi nitoe tu wito kwa Watanzania wenzangu kwa kweli tusipende kuyachezea chezea maeneo haya kwa sababu ni maeneo hatarishi sana.
Mheshimiwa Spika, kwa namna hiyo niombe tu yale maeneo tuliyoyabainisha kwa ajili ya matumizi ya jeshi wananchi wa kawaida tusipende kwenda kuvamia maeneo haya kwa sababu yamekuwa hayana matokeo mazuri kwa wananchi wengine wanaokota yale masalia ya mabomu, wanayachezea na wakati mwingine yanaleta madhara.
Mheshimiwa Spika, mimi sina maelezo marefu, tumuache mtoa hoja aweze kwenda kuhitimisha jambo lake, naomba kuwasilisha. (Makofi)