Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

Hon. Mwantumu Mzamili Zodo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

MHE. MWANTUM M. ZODO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nachukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia afya njema na kunifanya niweze kutekeleza majukumu ya kila siku.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nachukua fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uchapakazi wake na kuendelea kutatua changamoto za Watanzania katika nyanja zote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niendelee kumpongeza Waziri, Naibu Waziri pamoja na watendaji wote wa Wizara kwa uchapakazi wao na niendelee kuwapongeza sana kwa namna mnavyoendelea kupambana kutatua changamoto za mawasiliano katika maeneo yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye baadhi ya maeneo yetu bado kuna changamoto ya mawasiliano, kwa mfano katika maeneo ya Masagalu, Jimbo la Kilindi, Magoroto Jimbo la Muheza na maeneo ya Tanga Mjini. Niendelee kuiomba Wizara, muendelee kutukumbuka katika programu yenu ya minara 800.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia niishauri Wizara kuhakikisha maeneo yote ya taasisi za Serikali kama shule, hospitali, halmashauri na kadhalika yanakuwa na mawasiliano ya uhakika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.