Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilwa Kaskazini
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Mwenyekiti, natangulia kumshukuru Mhashimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwekeza miradi mikubwa ya mawasiliano ya simu za mkononi kupitia maradi wa minara 1,494 (758 plus 636). Nakupongeza Mheshimiwa Waziri Jerry Silaa na Naibu wako Mheshimiwa Maryprisca Mahundi kwa kazi nzuri mnazozisimamia katika Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati nilipoingia madarakani na kuwa Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kaskazini jumla ya vijiji 22 havikuwa na mawasiliano ya simu za mkononi. Ndani ya miaka minne jumla ya vijiji 13 vimefikiwa na huduma za mawasiliano ya simu za mkononi. Jumla ya vijiji vinne vya Nandete, Mwengei, Chapita na Pungutini vilifikiwa na mawasiliano ya simu za mkononi ya minara ya TTCL ya 3BG mwezi Agosti, 2021. Minara na Madishi ya GB4 na 5 ya Tigo na Airtel katika vijiji vya Kandawale/Namatewa, Kipindimbi, Mkarango na Chumo. Minara hi imeongeza mawasiliano ya simu za mkononi katika vijiji kumi na vitatu. Aidha ipo miradi inayoendelea katika vijiji ya ujenzi wa minara ya TTCL na Tigo. Vijiji hivyo ni MT Kimwaga (Narayan), Miumbu/Mtyalambuko, Zinga Kibaoni (Nambunju), Marendego, Kandawale, Miguruwe/Mtepela na Ingirito. Miradi hi imepangwa kukamilika mwishoni kwa mwezi Mei, 2025. Itakapokamillika jumla ya vijiji 18 vitakuwa vimefikiwa na mawasiliano ya simu za mkononi ndani ya kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan na vitabaki vijiji vinne vya Hanga, Ngarambi, Nambondo na Mtende.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri kwa Serikali; kwanza minara ya GB3 ya TTCL Nandete, Pungutini, Chapita na Mwengei ifungwe mitambo ya GB 5/4.
Pili, vijiji vinne vya Hanga, Ngarambi, Nambondo na Mtende vipelekewe miradi ya minara ya simu za mkononi ili kumaliza changamoto ya mawasiliano ya simu za mkononi; tatu, mnara wa mawasiliano ya redio wa Nangurukuru ukamilishwe na mnara wa redio wa Mlima Kitope uboreshwe ili kuimarisha mawasiliano ya redio Kilwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nne, nakuomba Mheshimiwa Waziri tuambatane pamoja tukazindue mnara mmoja wa Kipindimbi mara baadaya Mheshimiwa Rais kufanya uzinduzi wa Kitaifa wa minara 758.