Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hotuba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoitoa wakati wa Ufunguzi Rasmi wa Bunge la Kumi na Tatu, Tarehe 14 Novemba, 2025

Hon. Dr. Wilson Charles Mahera

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Hotuba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoitoa wakati wa Ufunguzi Rasmi wa Bunge la Kumi na Tatu, Tarehe 14 Novemba, 2025

MHE. DKT. WILSON C. MAHERA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa nianze kukushukuru kwa kunipatia fursa nami kuweza kuchangia katika mjadala huu wa leo. Kwa vile ni mara yangu ya kwanza kusimama hapa Bungeni ili kuweza kuchangia, ninaomba kwanza nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa baraka nyingi alizonipatia hadi kunifanya niwe Mbunge katika Jimbo la Butiama na kuwa Mbunge katika Bunge letu hili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, ninachukua nafasi hii kumshukuru Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ni Rais wetu na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi pamoja na vikao vya juu kuniamini na kuniteua kwenda kugombea Ubunge katika Jimbo la Butiama na ninapenda pia wananchi wa Butiama kwa kura nyingi za kishindo ambazo walipatia CCM katika ngazi ya Urais. Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan alipata 98% katika Jimbo la Butiama nami nilifuatia kwa kupata 97%, lakini kata zote 18 ziko kwa tiketi ya CCM. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wa Butiama walikuwa wana sababu za kufanya hivyo. Butiama imeanzishwa mwaka 2013, lakini kwa muda mrefu kumekuwepo na changamoto kwenye baadhi ya miradi, lakini Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan alipoingia kwa muda wa miaka minne ameweza kutupatia zaidi ya shilingi bilioni 345. Haikuwa jambo dogo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, amefanya mambo mengi makubwa katika Sekta ya Afya. Tuna kata 18, lakini wakati anaingia tulikuwa na kata tatu na yeye katika kipindi chake pia tumepata kata tatu zenye vituo vya afya, lakini sasa hivi tumeongeza katika kipindi chake vituo sita vya afya, hilo siyo jambo dogo. Katika kipindi chake pia ameweza kujenga zahanati 14, shule nyingi za msingi mpya na za sekondari na madarasa, matundu ya vyoo na mabweni yamejengwa katika kipindi chake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu sekta ya maji; tulikuwa tuna shida ya maji katika kata zote 18, kata mbili tu ndiyo zilikuwa zina uhakika wa kupata maji safi na salama, lakini katika kipindi chake kuna mradi wa maji wa shilingi bilioni 70.5 ambao tayari umeshakamilisha miundombinu ya msingi na unaenda kutupatia maji katika maeneo mbalimbali. Hata hivyo, kilichosalia sasa ni kutafuta fedha kwa ajili ya kuweka mtandao wa maji. Ninadhani hili Mheshimiwa Rais ameshaahidi. Tayari nimeongea na Waziri wa Maji; ameahidi kuna mradi wa usambazaji maji ambao ni wa thamani ya shilingi bilioni 4.8, ukipatikana huo wananchi wataweza kupata maji kwenye maeneo kama ya Kata ya Mirwa, Buhemba, Muliaza na Busegwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Butiama pia tumepata Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere chenye thamani ya shilingi bilioni 102. Hiki chuo kitaongeza thamani sana katika maisha ya wananchi wa Butiama katika masuala ya ajira za muda mfupi na ajira za muda mref,u lakini pia wananchi wa Butiama na hasa kanda ya ziwa wataweza kusoma kwa karibu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi chake hicho vilevile tumepata fedha shilingi bilioni 10.7 kwa ajili ya TARURA, shilingi bilioni 14.9 kwa ajili ya masuala ya TASAF. Hizo zote ni sababu za msingi ambazo zimepelekea Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kupata kura 98% kwenye Jimbo la Butiama. Katika siku zake 100 tayari Wilaya ya Butiama tumepata watumishi 80 wapya kati ya hao 80, 50 ni walimu wa shule za sekondari. Vilevile, tumepata watumishi 27 wa sekta ya afya, watumishi wawili kwenye Kilimo na Mifugo na mmoja upande wa Mipango. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye sekta ya nishati tuna vitongoji 160 ambavyo havina umeme, lakini katika siku zake 100 tayari vitongoji 51 vinakwenda kupata umeme, kwa hiyo vitongoji 119 vilivvyosalia maana yake ni kwamba kabla ya mwaka 2030 vitongoji vyote vitakuwa na umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo sasa, ninaomba sasa nijikite kwenye hotuba ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, hotuba ambayo imesheheni matumaini makubwa na mipango madhubuti ya kwenda kuibadilisha nchi yetu ya Tanzania. Ili uweze kuwa na maendeleo ni lazima wananchi wa nchi husika wapate elimu ya kutosha na hasa upande wa sayansi, teknolojia na uvumbuzi. Kwa hiyo, ukiangalia Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliielekeza Wizara ya Elimu kufanya mabadiliko ya kuboresha sera pamoja na mitaala ili kuweza kuweka mkazo zaidi katika elimu ya ujuzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii inakwenda kujibu hoja ya watu kumaliza elimu ya msingi au sekondari wanakuwa hawana ajira na hii katika sera na mitaala pia ilivyobadilishwa maana yake elimu ya lazima sasa ni miaka 10. Kwa hiyo, ina maana vijana wetu itakapofika mwaka 2030, tutakuwa na graduates wengi sana wa form four na form six.

Mheshimiwa Mwenyekiti, imeelekeza pia katika masuala ya elimu ujuzi ukiangalia kwenye hotuba yake ukurasa wa 19 anasema: katika kipindi cha miaka mitano anakwenda kuweka msisitizo zaidi katika utekelezaji wa elimu ujuzi. Pia, tunamshukuru Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kujenga VETA nyingi nchini Tanzania. Tunachokiomba kwa sasa ni kuhakikisha kwamba Serikali inatafuta fedha ili kukamilisha zile VETA 65 ambazo zinajengwa, lakini pia tupate fedha za kununua vifaa kwa ajili ya kujifunzia na kufundishia, ambapo sasa hivi kwa mtaala mpya ni kwamba elimu ni nyumbufu baadhi ya wanafunzi wanakwenda kwenye mikondo ya amali na wengine wanakwenda kwenye mikondo ya kawaida. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuonesha kwamba sasa anakwenda kutatua tatizo la ajira nchini ameamua kujenga shule za sekondari 830 katika kipindi cha miaka minne iliyopita na kati ya hizo shule, shule 103 ni shule za amali na shule 29 ni shule za amali za kihandisi (technical schools) kama ulivyokuwa unasikia Moshi Technical School. Sababu tunakwenda kuwa nazo shule 29, hilo siyo jambo dogo. Kuna shule 74 za amali zisizo za kihandisi na shule 694 ni shule za sekondari za kata. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia kwenye hotuba hapa alisema anakwenda kuweka msisitizo zaidi katika masuala ya sayansi na hisabati na hasa kwa wasichana. Tayari Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshajenga shule 26 za wasichana katika mikoa yote 26. Hilo siyo jambo dogo, lakini na tayari shule za kikanda saba kwa ajili ya wavulana zinajengwa na anataka kujenga shule katika kila mkoa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa haya yote ukiyaangalia kwenye elimu ya ngazi ya awali, madarasa mengi ya awali, sekondari, msingi pamoja na vyuo vya kati yanajengwa kwenye nchi yetu. Sasa kwenye elimu ya juu napo amefanya mambo mengi makubwa ambayo kwa kweli watu wengi hawayafahamu, lakini ni makubwa sana. Kila mkoa kwa sasa unakwenda kuwa na kampasi za vyuo vikuu maarufu hapa nchini, hilo siyo jambo dogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo ni kampasi za vyuo kama vile vya Mzumbe, SUA, University of Dar es Salaam na Arusha Institute of Accounts kwenye mikoa 15. Hivi vyuo vitaongeza fursa kwa vijana wetu ambao watakwenda kusoma kwenye hivi vyuo lakini pia ni fursa kwa ajili ya ajira ndogondogo na zitatumika pia kuandaa vijana ambao watakwenda kuwa walimu katika shule zetu za amali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kwa sababu anasisitiza elimu ya ujuzi kuna mradi mkubwa wa US Dollar milioni 90 kwa ajili ya kukuza ujuzi katika nchi za Afrika Mashariki. Hapa vinajengwa vituo vinne vya umahiri ambavyo kwa Kiingereza inaitwa centre of excellence. Ukiangalia pale Dar es Salaam, Institute of Technology kuna kituo cha umahiri kwa ajili ya mafunzo ya TEHAMA na hii maana yake ni maandalizi kwa ajili ya kwenda, watu wetu kwenda kujifunza masuala ya akili unde.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapohapo kwenye kampasi hiyo, kwenye Taasisi ya Dar es Salaam kuna chuo kipo Mwanza ambapo watu watafundishwa mafunzo ya umahiri kwa ajili ya uchakataji wa ngozi. Pale Arusha Technical College kuna Kituo cha Umahiri kule Kikuletwa ambacho hiki kina focus katika masuala ya utafiti wa nishati jadidifu, ambavyo vyote hivi vinakwenda kuandaa vijana wetu ambao watasoma kwenye shule za amali kuweza kubobea katika masuala ya ujuzi ili kuweza kuibadilisha nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwa kifupi ninataka kusema haya anayoyafanya Dkt. Samaia Suluhu Hassan, kwa sababau kama nchi ili kuweza kuendelea lazima tujiulize tulikuwa wapi, tuko wapi na tunakwenda wapi? Mwanzoni kabisa tulitangaza kwamba tuna maadui watatu: maradhi, ujinga na umaskini na njia ya kupambana na umaskini ni kuwasomesha vijana. Kwa hiyo, ukiangalia fursa zote hizi maana yake vijana wetu wa Kitanzania wengi sasa hivi wakae mkao wa kusoma na mkao wa kupata ujuzi mbalimbali wa kuweza kujiajiri wao wenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili haya yaweze kufanikiwa tunatakiwa kuwa na amani na utulivu katika nchi yetu. Hayo mageuzi makubwa ambayo yamefanyika sasa hivi katika utekelezaji wa sera na miataala mipya yanahitaji fedha nyingi sana, ndiyo maana kwa muda mrefu tangu mwaka 1974 tulipokuwa tuna falsafa ya elimu ya kujitegemea wengi tulishindwa kutekeleza hilo kwa sababu ya gharama kuwa kubwa sana, lakini Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan alithubutu na amedhamiria kuibadilisha nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, ninaomba sasa niunge mkono hoja ya Serikali, ahsante sana. (Makofi)