Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hotuba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoitoa wakati wa Ufunguzi Rasmi wa Bunge la Kumi na Tatu, Tarehe 14 Novemba, 2025

Hon. Eng. Mwanaisha Ng'anzi Ulenge

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Hotuba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoitoa wakati wa Ufunguzi Rasmi wa Bunge la Kumi na Tatu, Tarehe 14 Novemba, 2025

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa nafasi ya kuchangia. Awali ya yote nimshukuru Mwenyezi Mungu mwenye enzi na utukufu ambaye amenijalia mimi kuwa miongoni mwa wale ambao wamepata kibali cha kurudia Bunge hili kwa awamu nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kipekee kabisa ninawashukuru sana ndugu zangu, wananchi wenzangu, wanawake wa Mkoa wa Tanga kwa kujitendea haki kwa kunichagua mimi mchapakazi jembe ambaye hakika sitaitweza thamani waliyonipa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nichukue fursa hii pia kuchangia hotuba hii tukufu ya Rais wetu mpendwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyoitoa tarehe 14 Novemba, 2025 akilihutubia Bunge hili Tukufu, akitekeleza matakwa ya Kikatiba kama yaliyotajwa katika Ibara ya 91(1). (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba niseme kwamba Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa hotuba, hotuba nzito yenye mwelekeo chanya kwa mustakabali mpana wa Taifa letu la Tanzania. Ametoa hotuba nzito yenye kutuweka pamoja, yenye kutengeneza umoja wa Kitaifa, yenye kusisitiza amani na utulivu wa Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan hakika ameweka kiwango na rekodi ya juu sana. Hotuba yake aliyoitoa tarehe 14 Novemba nimeifananisha na hotuba iliyowahi kutolewa na Margaret Thatcher, aliyekuwa Waziri Mkuu mwanamke wa Uingereza mwaka 1979 baada ya kushinda uchaguzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Margaret Thatcher na yeye katika hotuba yake ile alihimiza umoja na mshikamano. Ninaomba nirekodi kwamba Margaret Thatcher alisema: “Where there is discord may we bring harmony, where there is error may we bring truth, where there is doubt may we bring faith, and where there is despair may we bring hope”. Maneno haya ni sawa sawa na maneno aliyoyazungumza Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akitutaka kama Taifa tujirekebishe, tujielimishe na tuboreshe demokrasia yetu kwa kufuata misingi na tamaduni zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, huyo ndiye Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye kwa hakika ameweka rekodi kama mwanamke kiongozi bora katika dunia hii. Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo ametekeleza majukumu yake, hapana shaka kiwango cha Margaret Thatcher ameshakipita. Hakika mwanamama huyu amefanya mambo makubwa katika Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamtia moyo kwa maneno ya kitabu kitakatifu, kitabu cha Quran. Kuna mahali panasema “Falaa yahzunka qawluhum; innaa na‘lamu maa yusirruna wa maa yu‘linuun.” kwamba, “Yasikuhuzunishe maneno yao, hakika sisi tunajua yaliyojificha na yaliyo wazi”. Mungu wa Mbinguni ambaye anaiona kazi kubwa ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, nina hakika yuko pamoja naye na ataendelea kumlinda na Tanzania itaendelea kusimama katika viwango vya juu kabisa ndani ya dunia hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Rais wetu mpendwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mambo makubwa na sisi Mkoa wa Tanga tulikuwa na kila sababu ya kumjazia kura nyingi za kishindo. Hakika mama huyu kwanza kabisa ametutoa kimasomaso wanawake wa Taifa hili. Kila aliyekuwa aki-doubt sasa hivi anaona haya kwa namna ambavyo amewa-outshine kwa kazi nzuri na kubwa ndani ya Taifa letu. Nani kama Mama Samia? (Makofi)

MBUNGE FULANI: Hamna.

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mama Samia hakika jamani sisi wananchi wa Mkoa wa Tanga ambao tulikuwa na viwanda, viwanda kadhaa ambavyo vilikuwa vimekufa, nami mwaka 2024 hapa niliomba katika Bunge hili Tukufu viwanda vile viweze kufufuliwa, lakini ndani ya siku 100 za Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan tayari Tanga viwanda vitatu vimekwishakufufuliwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi vijana na wananchi wa Mkoa wa Tanga tunaona fahari kubwa sana kwamba hatukukosea sisi kumpa kura nyingi kwa namna ambavyo tumempa, 98% Mama Samia zinamstahili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndugu zangu sisi wananchi wa Mkoa wa Tanga Kiwanda cha African Harmony kimetoa ajira za kudumu kwa vijana 218. Kiwanda ambacho kimekufa muda mrefu sana tangu enzi za Nyerere, leo Mheshimiwa Mama Dkt. Samia amekuja kuirudisha rekodi ya Nyerere na kuirudisha ramani ya Mkoa wa Tanga. Tuna kila sababu ya kumwombea heri na baraka nyingi Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mama yetu huyu, kiwanda kingine cha Rolling Steel ambacho kinatengeneza nondo, kiwanda ambacho kinazalisha nondo takribani tani 30 mpaka tani 40 kwa wiki, leo Tanga kimeanza kufanya kazi ndani ya siku 100 za Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Nani aseme kwamba eti Mhehsimiwa Dkt. Samia sijui ajiuzuru? Tutamjibu kwa hotuba ya Margaret Thatcher alisema: “There is no turning back. The lady should go on; the lady is not weak; the lady is capable enough.” Tunampongeza sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kiwanda kingine cha Plywood kinachotengeneza marine board na Plywood Tanga tayari kinaanza kufanya kazi ndani ya siku 100 za Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Mioyo yetu imejawa na unyenyekevu, imejawa na shukrani dhidi ya Mama huyu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunampongeza sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Kwa hakika ametusaidia wanawake wa Mkoa wa Tanga, leo hii tunabeba maji majumbani kwetu kwa kiwango kikubwa sana. Ametuletea shilingi trilioni tatu katika miaka yake minne ya uongozi wake. Shilingi trilioni tatu hizo hazijawahi kutokea tangu Tanga imeumbwa. Tuna kila sababu ya kumwagia kura nyingi, kura nyingi za kishindo na hakika Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan bado dhamira yake ya kuleta ufanisi kwa wanawake wa Mkoa wa Tanga imeendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pale ndani ya Wilaya ya Mkinga ametuletea juzi tu vifaa mwa! mwa! kwa ajili ya maji, shilingi bilioni 35 zimeshuka ndani ya Wilaya ya Mkinga. Nani kama Mama Samia Suluhu Hassan? Hakika tuna kila sababu ya kuuona mwelekeo wake chanya alioutoa katika hotuba yake hii kwa mustakabali mpana wa Taifa letu. Sisi Wabunge kama alivyotuusia kwamba tuibebe dhamana tuliyopewa na wananchi ili tuweze kushauri ipasavyo, nasi tutamshauri Mama bila hiyana kwa sababu ni Mama msikivu, anayoyatekeleza mambo yote tunayoyaweka katika matendo. Tunakushukuru sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan vilevile katika hotuba yake upande wa elimu ameonesha umuhimu wa kuunganisha mikoa na wilaya kidijiti ili kubadilishana uzoefu na wanafunzi kuweza kupata maarifa endelevu. Sisi tunamshauri Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, jambo hili ni jema sana kuunganisha wanafunzi wa vijijini na mjini kidijiti kuweza ku-share uzoefu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ionekane haja ya kuitumia TEHAMA kupunguza wimbi la upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi. Kwa kutumia TEHAMA tunaweza kumfanya Mwalimu mmoja akafundisha madarasa matatu kwa wakati mmoja na hapo tutakuwa tumetatua changamoto ya walimu wa masomo ya sayansi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi wananchi wa Mkoa wa Tanga tunathamini sana kazi kubwa anayoifanya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Tunaahidi kwamba tutaendelea kuchapa kazi kumuunga mkono, kumsemea kwa dhati ya mioyo yetu. Tunaiona kazi njema, kazi anayoifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi tunaomba, kupitia yeye Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan tunaamini msamiati hauwezekani, haupo ndani kwa Mama Samia. Mambo yake yote yanawezekana na amefanya makubwa katika Taifa hili. Tuendelee kumwomba atuwezeshe Barabara yetu ya Kiomoni – Mlingano kilometa 35.9 ziweze kujengwa kwa kiwango cha lami. Barabara ile imeshikilia uchumi wa Mkoa wa Tanga. Siyo Tanga Jiji, bali uchumi wa Mkoa wa Tanga unashikiliwa na barabara ile kwa sababu ya the best limestone in Sub-Saharan African Countries ambayo inazalisha viwanda vile vya saruji vilivyopo Tanga. Tunaomba barabara hii ijengwe kwa kiwango cha lami ili kuvutia wawekezaji zaidi katika ukanda ule. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kushukuru, nimekuona umeshika mic yako sawasawa. Ahsante sana. (Makofi)