Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

Hon. Bupe Nelson Mwakang'ata

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante na ninashukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia katika Wizara hii muhimu. Kwanza kabisa nimtangulize sana Mwenyezi Mungu kwa kutujalia uzima na hatimaye tunasimama katika Bunge lako Tukufu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie nafasi hii kumpongeza Waziri dada yangu Mheshimiwa Jenista kwa kazi nzuri. Amekuwa ni mwalimu kwa sisi wanawake wenzake na anafanya kazi nzuri sana. Mimi katika Mawaziri bora, Mheshimiwa Jenista ni Waziri bora pia yumo. Ninakupongeza sana Mheshimiwa Waziri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze pia Naibu Waziri kwa kazi nzuri. Wamekuwa wakimsaidia vizuri sana Mheshimiwa Rais wetu mpendwa mama yetu Samia Suluhu Hassan. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze pia Katibu wa Wizara, watumishi wote na wataalam wote wa Wizara ya Afya kwa kazi nzuri wanazofanya. Pia, nimpongeze Mganga Mkuu wa Mkoa wetu wa Rukwa Dkt. Ibrahim Isack na Katibu wa Afya wa Mkoa kaka yangu Masusu Ramadhani. Wamekuwa ni msaada mkubwa sana kwa wanawake wa Mkoa wa Rukwa; kwa kweli wanafanya kazi nzuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kipekee nimpongeze sana Rais wetu mpendwa Mama yetu Samia Suluhu Hassan. Hakika mama amefanya kazi kubwa sana katika Wizara hii ya Afya. Wanawake tulikuwa na changamoto nyingi sana za afya, lakini mama amepunguza sana vifo vya mama na mtoto. Hongera sana kwa Rais wetu, aendelee kuchapa kazi, sisi tuko nyuma yako. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niingie kwenye Mkoa wangu wa Rukwa. Tunashukuru sana Serikali imetujengea hospitali za wilaya. Ndani ya kipindi kifupi tumepata wilaya nne, lakini bado tumepata katika Wilaya yangu ya Sumbawanga Vijijini. Juzi kati hapa katika kituo cha afya kipya tumepata shilingi milioni 700 katika Kituo cha Mbui na tumepata vifaatiba vyote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto kubwa ni wataalam. Mama amejenga, tumepata fedha nyingi sana za kujenga vituo vya afya, tumejengewa hospitali za wilaya na tumejengewa zahanati. Katika Wilaya yangu ya Sumbawanga Vijijini tumepata zahanati 18 kwa muda wa ndani ya miezi sita. Hongera sana Serikali yangu, hongera sana Rais mpendwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba Serikali yetu iangalie; wataalam wamekuwa ni changamoto sana. Tuna majengo mazuri, vifaatiba vimefika, lakini tatizo wataalam, madaktari bingwa hatuna. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Mkoa wetu wa Rukwa tuna upungufu mkubwa sana wa wataalam wa meno na wauguzi; ni changamoto kubwa sana. Tunaomba sana watakapokuwa wana-windup watuambie ni lini sasa wataalam wataongezeka katika Mkoa wetu Rukwa? Pia, specialists wa maabara hatuna, tunaomba sana watuangalie katika Mkoa wetu wa Rukwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni ushauri. Hapa katikati pamekuwa na wimbi la wafadhili, wafadhili walitia mgomo kuendelea kutuletea dawa. Ninaishauri Serikali yangu kwamba, tuendelee kujiwekeza, tuanzishe viwanda, tutengeneze viwanda vya kutengeneza dawa sisi wenyewe nchini, ili wafadhili wetu kama wakitia mgomo sisi wenyewe tuendelee kujiwekeza kutoa dawa kwa magonjwa mbalimbali, yakiwemo magonjwa ya TB, upungufu wa kinga na magonjwa mbalimbali ambayo yanaleta shida sana katika nchi yetu. Ninaomba tuanze kujiwekeza wenyewe kutengeneza, kujenga viwanda vyetu, tujitegemee wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine katika Mkoa wetu wa Rukwa ni tuna changamoto, siyo kubwa, lakini ni changamoto. Tulitenga eneo la kujenga hospitali ya rufaa, kuna sehemu inaitwa Milanzi, Serikali ililipa wananchi, wananchi wale waliachia lile eneo, lakini mpaka sasa bado ujenzi huo haujaanza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunashukuru, nimeona katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri ametenga fedha, tunaomba ujenzi huu aanze haraka. Kwa sababu, eneo lilipo tunalo eneo la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, limekuwa ni finyu na majengo yamekuwa ya zamani. Tunaomba lile eneo liendelee kutumika, hospitali yetu ya Rufaa ya Mkoa ujenzi uanze haraka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, ninashukuru sana na ninaunga mkono hoja. (Makofi)