Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

Hon. Anatropia Lwehikila Theonest

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia kwenye hii Wizara nyeti. Nitaanza kwa ku-quote, nitam-quote William Graham, huyu ni mwandishi wa vitabu na ni motivation speaker, alisema hivi: “When wealth is lost, nothing is lost; when health is lost something is lost; and when character is lost all is lost”. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ninaonesha mkazo kwenye wealth. Weath ni mali, weath ni utajiri, wealth ni uchumi. Unaweza kupoteza kila kitu lakini hujapoteza kila kitu. Ninakuja kwenye afya, ukipoteza afya kuna kitu kitakuwa kimepotea. Ukipoteza character kwa maana ya sifa kuna kitu au kila kitu kitakuwa kimepotea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwa nini nimeongea haya? Katika vitu vyote tunavyovifanya msingi wake ni afya, sisi tunao msemo unasema: “Kwa sababu nina nguvu nitapambana”, lakini ukipoteza kitu kinaitwa nguvu mapambano yote yamefikia ukingoni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninam-quote mzungumzaji ambaye amenitangulia, amesema: “Gharama ya matibabu hapo nchini ni ghali”. Nami ninaomba nirudie kwamba, ugharamiaji wa matibabu hapa nchini ni ghali sana. Katika kila tunachokifanya na katika kila tunachokifikiria tuwaze ni namna gani tunaweza kupunguza gharama ya matibabu hapa nchini. Haya yote nitayaongea leo utaona kwamba kutibiwa ni rahisi kwa sababu leo una fedha you have wealth, lakini ikifikia wakati ambapo hauna wealth na hauna health ndiyo utaelewa ninamaanisha nini nikisema gharama ya matibabu ni kubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo kama hauna chochote unaumwa ukaambiwa piga X-Ray, CT-Scan na Ultrasound ndiyo utaelewa ninamaanisha nini nikisema gharama ya matibabu iko juu. Siyo hiyo tu, ukiambiwa mwone Daktari kwa kiasi fulani, nenda kamwone daktari ukimaliza kumwona daktari nenda kwenye vipimo, ukatoka, nenda kwenye dawa rudi kwa Daktari, utaelewa gharama ya matibabu ni kubwa kiasi gani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwa nini tunafika hapa? Wakati mwingine nikifika kwenye hospitali hizi kubwa kubwa nikafurahia uwekezaji uliofanyika na Serikali za awamu mbalimbali nikasema kweli Watanzania wameweka kitu, kweli kodi za Watanzania zimefanya kitu na kweli zinaonekana kwa macho. Uwekezaji wa Watanzania uliofanyika basi return yake iwe upungufu au kupunguza gharama za matibabu ambazo wanapaswa kuzipata wakati afya zao zimetetereka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya ninayaongea nikilinganisha na vifurushi au package za bima ambazo leo tuko nazo na tunazi-market au Wizara imekuwa ikizisemea. Ukiangalia gharama za vifurushi leo tunavyoongelea kuna kifurushi cha Ngorongoro, Serengeti. Nikawa ninaangalia kwenye age group nikaona katika age kati ya 0 mpaka 17 unaona kwamba package ya vifurushi viko nafuu kidogo. Ukija kwenye age kati ya miaka 18 mpaka 35 unaona kwamba inapanda, unavyoendelea kupanda inakuja 36 mpaka 59 ambao pengine wengi wetu hapa ndiyo tuna-belong unaona kwamba inapanda. Mzani unavyoshuka kwanza wanasema sixty yaani ukianza kupanda ngazi ya sixty unaona kwamba gharama ya matibabu inaendelea kuwa kubwa zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mind you, hawa watu wa miaka 60 plus ni watu ambao leo hawana ajira, ni watu wamestaafu! Ni watu ambao hawana kipato, lakini huduma zao za matibabu ukiangalia kifurushi cha Ngorongroro mtu mmoja inakuwa ni shilingi laki saba na elfu nane. Serengeti ni shilingi 3,306,000. Unaona kwamba huyu Mzee ambaye najua gharama yake ya matibabu ni kubwa hakuna shida, lakini kwa miaka yake 60 ameshalitumikia hili Taifa. Hiyo miundombinu mnayoiona na majengo mnayoyaona, CT-Scan, ultrasound na yote yaliyonunuliwa ni kwenye kodi alizo-contribute kwenye miaka nenda miaka rudi. Kwa hiyo, ni lazima tuangalie tunapojadili hapa tufanye gharama za matibabu hapa nchini ziwe affordable, isiwe luxury. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna watu unawasikia, unaweza kukutana na mtu anasema, “Mheshimiwa Anatropia ninaumwa”, “Unaumwa kwa nini huendi hospitali?”, “Sina gharama za kwenda hospitali”. Ina maana kuna magonjwa mtu akipata yeye hatima yake ni kusubiri Mungu atakavyoamua, Mungu akiamua apone atapona, Mungu akiamua vinginevyo hata magonjwa ambayo angeweza kutibiwa hawezi kutibiwa ni kwa nini huduma za matibabu ziko aghali? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi wote tunaenda hospitali, huduma za bima za afya ni aghali, na hii tena ndiyo inaniumiza! Mtu anaweza kukata kifurushi cha shilingi laki sita au laki saba, yeye anajua akishakata bima kazi imeisha, ukifika unaambiwa kifurushi ulichokata dawa hizo hazipo! Hilo suala linaumiza Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninadhani Wizara wa5fanye computation ambayo inaweza kueleweka ambayo hata Serikali inaweza kui-facilitate kwamba mtu akikata bima ya afya ajue kwamba nimemaliza na niwekeze kwenye bima ya afya, kila mwaka nilipie ni-renew ili nitibiwe kwa sababu there is no guarantee kwamba nilivyokata kwenye mwaka husika nimeumwa, sasa kwa nini siku nikiumwa niambiwe hizo dawa hazipo kwenye hii package ziko kwenye hii package ambayo hukukata? Ninadhani ni kitu ambacho hakiko sawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine ambacho ninataka kukileta kwenu ningetaka Mbunge anayeweza kusimama hapa kwenye hii podium akasema yeye kwenye Jimbo lake mama mjamzito anatibiwa bure, yaani anapofika na tumbo lake anatibiwa anaenda nyumbani, anyanyuke hapa wapiga kura wake wamwone. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sera ya Afya ya Mwaka 2007 inayosema, huduma ya Mama Mjamzito na watoto chini ya miaka mitano itakuwa bure, haitekelezeki! Serikali iseme wazi. Tusiwadanganye akinamama tunapoenda kwenye majukwaa na tunapoenda majimboni tunaishia kusema maneno ambayo ni ya uwongo. Tunaanza kujichanganya! Tuwaambie ukweli kwamba ukienda hospitali nenda na taulo lako, nenda na gloves zako, nenda na vile vifaa vyote vya kujifungulia.

MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, Taarifa.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini hizi habari za kusema kwamba vitakuwa ni bure siyo kweli! Tuwaambie wananchi ukweli. (Makofi)

MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa wapi?

MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa kwa Mwenyekiti wa Kamati, Kingu.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Kingu.

TAARIFA

MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimpe taarifa dada yangu na rafiki yangu ninayempenda sana na kwa kweli anachangia kwa uzalendo mkubwa, ni Mbunge makini sina shida naye.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimpe taarifa kwamba rekodi zinaonesha kwamba kwa mwaka wa fedha uliokwisha wazee zaidi ya milioni 3.4 wametibiwa bila malipo kwa mujibu wa statistics za Serikali. Kwa hiyo, kusema kwamba sheria hii ya kuwatibu wazee na akinamama kwamba haitekelezeki ndiyo tunaweza tukawa na changamoto katika Taifa letu, lakini kwa kiwango kikubwa sana Serikali ya Chama Cha Mapinduzi imeendelea kutekeleza kuwasaidia wazee huduma za matibabu bila malipo, statistics hata tulipokuwa tunasomewa utekelezaji wa Ilani, moja ya vitu ambavyo Rais ame.......

MWENYEKITI: Ahsante.

MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Theonest, unapokea taarifa hiyo kutoka kwa Mheshimiwa Kingu?

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninawapongeza sana Wazee wa Jimbo lake ambao wamenufaika na hayo matibabu, lakini ninawaomba wasipewe matibabu Wazee wa Jimbo lake la Singida, Wazee wa Kyerwa pia wapewe matibabu hayo, kwa sababu nina uhakika pengine aliowataja milioni tatu siyo takwimu tu ninadhani wazee wanazidi hiyo takwimu, pengine ni wa kwake wamenufaika.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachotaka kusisitiza hapa, kama huduma ni bure tunaelewa ni kwa nini sera imekuja namna hiyo, ni kwa sababu ya umahsusi wa kundi husika, umahsusi wa akinamama wajawazito, umahsusi wa watoto chini ya miaka mitano. Kwamba kama ukizuia hili kundi, kama ukitanguliza fedha kwenye hili kundi, risk ni kwamba wanaweza kuacha kwenda hospitali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tutaendelea kuwatoza fedha risk itabaki palepale. Kwa hiyo, kama tunataka tuondoe risk hizo delivery kit tuzi-offer for free, na nina uhakika Serikali ikiamua inawezekana kabisa na tukajua kwamba tunavyoenda kujifungua we are free tunajifungua, hiyo tutakuwa tunasema tumeweza katika hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba niende kwenye jambo jingine kuhusu suala la malaria. Hakuna kitu kinasikitisha katika karne tuliyonayo leo bado tunaongelea changamoto ya malaria. Ukisoma hotuba ya Wizara ukasoma na randama inaonesha gharama ambazo zimewekwa kwenye kupambana na malaria. Ninataka nisome kidogo tu kwenye randama, inasema mapambano dhidi ya malaria, Wizara ilinunua na kusambaza dozi milioni nne za dawa mseto, dozi za malaria, dozi za sindano mahesabu yako hapa ya kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ninajiuliza kweli katika karne hii tunapaswa kuendelea kupambana na malaria? Ni kwa nini ninasema haya? Serikali ilifanya uwekezaji mkubwa wa kiwanda cha viuatilifu unaitwa biotech product kwa ajili ya kuchukua zile dawa kusambaza na kuua vimelea vya malaria. Ni kwa kiwango gani hizo dawa tumezinunua na kuzisambaza kwenye Halmashauri ili tuondokane na changamoto ya malaria? Leo malaria wanasema ni killer disease, inaua kwa 33% ukilinganisha na magonjwa mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajua tuna uwezo wa kupambana na malaria lakini hatupambani na malaria. Tunaongelea vyandarua, tumesambaza vyandarua kadha wa kadha kwenye Mikoa lakini kwa nini tusiongelee tumesambaza zile dawa za kupambana na vijidudu vya malaria? (Makofi)

WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Waziri, Jenista Mhagama.

TAARIFA

WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kwamba tutasubiri ili tuweze kutoa majibu ya kina, lakini katika maeneo ambayo Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan amevunja rekodi na kufanya vizuri sana na kwenye hotuba yangu nimeiweka wazi labda Mheshimiwa Mbunge hakupata nafasi ya kupitia, ni pale alipoingia madarakani na kuamua kuhamisha nguvu ya mapambano dhidi ya malaria kwenye udhibiti na kuendelea na tiba pia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeshatoa shilingi bilioni 10 na tumekwishanunua zaidi ya lita laki 833.333 za dawa ya kuua viutilifu ambavyo vinazalisha mbu wa malaria. Kwa hiyo, jambo hilo tayari Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imeshafanya hiyo kazi. Dawa zimeshasambazwa na sasa hivi tunasubiri mvua ziishe dawa zitaanza kunyunyizwa kwenye halmashauri zote nchini.

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Waziri. Mheshimiwa Anatropia taarifa hiyo unaipokea?

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikiipokea sasa hivi atajibu nini wakati wa ku-wind up? Wakati wa ku-wind up anapaswa kujibu hayo niliyoya-raise kwenye mjadala. Ninataka kusema hivi, tangu tumekuwa na kiwanda pale Kibaha zaidi ya miaka nane, leo tungekuwa tunaongelea changamoto ya malaria? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tungekuwa leo tunawekeza fedha kwenye vyandarua? Tungekuwa leo tunajivunia kununua zile rapid test kadhaa? Kupanga ni kuchagua! Yeye ni Waziri wa Wizara hii na anafanya kazi, anafanya kazi, anapambana! Kwa hiyo, akiamua kununua zile dawa akazisambaza, leo hatutaongelea tena vyandarua.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Anatropia ulitakiwa ukatae au ukubali hiyo taarifa, lakini malizia mchango wako.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ananipotezea muda. Ninapokea kwamba sasa wanaweka mikakati, tunaanza kuona tukitokomeza malaria, tunaacha biashara ya chandarua, tunaacha biashara ya kuuza dozi za malaria kwa maana ya kuhangaika na hizi dawa wakati tuna uwezo wa kutokomeza malaria kupitia kiwanda ambacho tunacho nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuliweka fedha tumewaleta watu wa Cuba na badala yake nilikuwa hapa, kuna ziara kuna baadhi ya wanasiasa huwa wanafanya ziara kwenye hicho kiwanda halafu wanawaeleza wale wa kiwanda kwamba fanyeni jitihada za kujitangaza. Hivi kweli leo tunakiambia kile kiwanda kujitangaza? Au sisi ni kazi yetu kukitangaza na kuuza zile products kwenye nchi mbalimbali zinazotuzunguka ambazo pia zinapata changamoto ya malaria? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa kama muda wangu upo, nitaongea kwa kusikitika tena.

MWENYEKITI: Muda wako umeisha na nilikuwa nimekuongezea kidogo, muda wako umeisha.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana. (Makofi)