Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2024 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026; na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

Hon. Dr. Charles Stephen Kimei

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vunjo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2024 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026; na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Nami nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Rais na wasaidizi wake, Waziri wa Fedha, Naibu wake, pamoja na Waziri wa Mipango na Uwekezaji, kwa kutuletea Mpango mzuri na bajeti nzuri kwa mwaka unaokuja wa 2025/2026.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nikikumbuka kwamba kweli huu ndiyo mchango wangu wa mwisho kwenye bajeti hizi za hili Bunge la Kumi na Mbili, mchango kwenye bajeti kuu ambayo naanza kwa kusema ninaunga mkono, nasema pia nawiwa kuwashukuru wananchi wa kule Vunjo kwa kunichagua kuwawakilisha kwenye Bunge hili, na ninaamini wanaridhika na wataridhika kwamba nimewatendea haki kwa kupigania sehemu ya kutosha kwenye ugawaji wa keki hii ya Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naamini pia kwamba tunaunga mkono kwa sababu kuna miradi inaendelea. Miradi hiyo inajumuisha kuweka kwa kiwango cha lami barabara ile ya Pofo – Mandaka – Kilema, Barabara ya Uchira, Kisomachi – Kolarie, Chekereni – Kahe – Mabogini ambayo Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI aliipa shilingi bilioni saba siku za karibuni alipotembelea kule. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme hivi nami nianze hapa kwenye RND kwa sababu naona imezungumzwa na kila mtu kwa namna moja, lakini watu wanafikiri kwamba RND ni muhimu tu kwenye sayansi (Fundamental Sciences), lakini ukweli ni kwamba RND utafiti unahitajika sana kwenye kusaidia kutunga sera za maendeleo ya jamii na uchumi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa bahati mbaya Bunge hili au wizara zinazohusika hazijatilia maanani kwamba tuna taasisi kama REPOA, SRF, Uongozi Institute, na kuna taasisi nyingine ambazo zinafanya fundamental research ambayo itasaidia pia hususan kutengeneza mipango ambayo iko evidence based na decision zifanyike kwa kutegemea na kwa kuchukulia mahitaji na matakwa muhimu ya jamii yetu kwenye maeneo mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba katika utekelezaji wa bajeti inayokuja, Mheshimiwa Waziri wa Mipango, alinihakikishia kwamba ameweka vote kidogo, lakini naomba hizo igawe vizuri kila taasisi iliyopo iweze kunufaika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye maeneo yote mawili; Bajeti na Mipango wamezungumzia issue ya hali ya Uchumi, na akasema hapa tuna global by 5.5% kwenye mwaka huu wa 2024. Ninashukuru kwamba hiyo ni achievement nzuri na ni ya kupongeza wahusika na kupongezwa Watanzania kwa ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme kwamba siyo tofauti sana na nchi nyingine za East Africa Community kwa sababu ni zina-grow kwa wastani wa 5% wenyewe ukiondoa Sudan. Sudan ilianguka kwa 27.6% na tunajua sababu. Kwa hiyo, tunapojilinganisha, tuangalie kwamba hatujawa mbali, lakini tunaweza kuwa mbali kwa sababu tulikuwa tumewahi kufikia ongezeko la 7.5%.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naseme hivi, pamoja na hivyo, kinachofurahisha au pia kinachokuwa changamoto ni kwamba ongezeko la pato la Taifa hapa kwetu limechangiwa zaidi na uwekezaji wa Serikali. Kwenye maeneo yale ambayo tunashangilia miundombinu, usafirishaji, mambo yote yanayohusika na infrastructure, so to speak. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, private sector inaonekana imedumaa, yaani uchangiaji wa private sector bado ni mdogo sana. Sasa ninachouliza ni hivi, tungejiuliza zaidi ni kwa nini na sababu zipo zinajulikana? Juzi Mheshimiwa Profesa Jeffery Sachs ambaye ni mmoja wa maprofesa mashuhuri duniani katika masuala ya uchumi. Alisema kwamba, ili kuwezesha nchi za Afrika ziweze kukua kwa zaidi ya asilimia saba inahitaji vitu vitatu au kitu kama hicho ni entrepreneurship na ubunifu, tunahitaji mikopo ya muda mrefu na yenye riba ndogo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa issue inageuka, kwa nini mikopo haipatikani? Hiyo mikopo inaweza ikapatikana, watu wanasema hakuna sources, lakini naamini kwamba mikopo hiyo inaweza ikapatikana kama tukilenga zaidi kwenye ku-improve efficiency ya financial system yetu na tukaifanya i-deepen zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, of course hatuwezi kutegemea tu benki za maendeleo zianzishwe na Serikali, lazima iweze kuvutia kwamba benki za nje au benki zilizopo zinaanzisha madirisha au subsidiary au kampuni tanzu za kuweza kutoa mikopo hii ya muda mrefu (investments banking in a group).

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba hivi, cha kwanza ni haya mabenki. Hata kama tunataka kusaidia mabenki, lazima yaongeze mitaji, na mitaji wa mabenki haitoki from nowhere. Yaani mitaji mingi ya mabenki inatoka from growing organically, maana yake ku-retain profits. Utakuta hapa mabenki yanapata profit kubwa, lakini wanagawa kigodo, wanabakiza the rest ili ikuze mitaji yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hela iliyoko kwenye benki kama shareholder funds ndiyo zinaweza zikatumika kukopesha kwa muda mrefu. Kwa sababu hizo ni home permanent; ni permanent source of funding, ni mitaji ile watu wamefanya paid up capital in equity. Kwa hiyo, inabaki forever na retain end zinakuwa ni sehemu ya shareholder funds ambazo zinaweza zikatumika kusaidia kukuza mitaji na ukopeshaji wa muda mrefu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nashangaa kwamba tumeingiza kodi ya withholding tax kwenye retain ends. Namwomba Mheshimiwa Waziri wa Fedha, anajua vizuri sana kama benki iki-retain au kampuni yoyote iki-retain fedha ikaongeza kwenye mtaji wake kwa kupitia plough back, halafu wakasema haa, lipa withholding tax kwa sababu hujagawa, basi ina maana kwamba corporate tax inakuwa 40%, 10% plus 30% ambayo wameshalipa kwenye profit yao. Ni kwamba wewe umewatoza kodi ya 40%. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kodi ya 40% hapa kwenye kanda hakuna wenzetu hapa wa kwenye East Africa Community wamepunguza corporate tax, zinakwenda mpaka 25%, 15%. Kwa hiyo, sisi tutajiondoa kabisa katika ushindani wa uwekezaji kwa sababu watu hawatawekeza wakijua watalipa 40% badala ya 30% au chini yake kwa sababu wenzetu wanashindana na sisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba hilo liangaliwe, lakini liangaliwe pia in the context kwamba hiyo inasaidia kuongeza uwezo wa mabenki yetu kukopesha kwa muda mrefu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo lingine ambalo tunaliona kwa sasa, okay unayo fedha ya kukopesha muda mrefu, lakini riba ni ndefu, ni 16 plus au mpaka 20. Sasa how do we go ahead addressing the challenge. Nafikiri challenge ya riba tumekaanayo muda mrefu. Kwa nini? Kwa sababu mabenki yamepewa facilities zote na incentives zote za kupunguza riba, lakini hayapunguzi riba. Riba zimebakia pale pale 16%, na tukiwauliza wanapata faida; mabenki yamepata faida ya trillions ukijumlisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nafikiri kwamba zile incentive tunazotoa hazisaidii kwa sababu kuna mtu anayetoa dhamana za Serikali akaipa kuponi ambayo ni 16% na anatangaza kabisa kwamba mimi nauza dhamana za Serikali kwa riba ya 16%, kila mtu anakimbilia kule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa mabenki yanasema kuwa sisi twende huko, tuanze kukimbizana na private sector! Private sector ambayo risks yake ni kubwa, anything can happen. Covid inaweza ikaja, tena nini wanasema hapo, ni hapo hapo, wanashikilia pale. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata mimi, nawekeza kwa sababu kwa nini nikampe mtu. Hata ndugu yangu nimpe hela akatupe tupe huko; naweka kwenye dhamana ya Serikali kwa sababu riba ni kubwa. Sasa issue ni kwamba how do you go ahead? Lazima tubadilishe mfumo, options za dhamana za Serikali za bonds, maana yake usitangaze bei, usitangaze riba ya kuponi, ile riba, riba ya ile kuponi kwa sababu utaleta mtu, anajua lakini sasa wasipojua unasema hee! Sasa mimi niki-bid above 10% sitauziwa, watauziwa wale ambao wame-bid below. Kwa hiyo, kila mtu amekuwa kwenye uncertainty. Kwa hiyo, kila mtu anayetaka kuwekeza, anabuni riba ambayo ni acceptable. Sasa ninyi mnaitangaza, sijui mimi nafikiri hapo hapafai kabisa, twende kitofauti kabisa. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme hivi, turudi kwenye mfumuko, exchange rate. Exchange rate, tunapongeza sana kusema kweli, kazi iliyofanyika na Wizara na Benki Kuu ni ya kupongeza, kwa sababu unajua imeserereka hivi; sisi yetu imeshuka mwaka uliopita 2024 kwa asilimia tisa. Sasa sikiliza, ya Kenya imeshuka kwa 16.3%; ya Uganda kwa 47%; sisi haijafika huko, si watu wange-riots hapa tungepata GeZ hapa watusumbue sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, bado tupo, imeshuka kwa asilimia tisa tu. Halafu Rwanda imeshuka kwa 48%, Burundi kwa 32%. Kwa hiyo, nafikiri ni vizuri wamefanya, lakini pia hata kushuka kwa asilimia tisa ni very easy to compare to others.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme kwamba pengine tungeweza pia kuangalia tukawa more flexible katika ku-manage exchange rate kwa kuruhusu periodic movement iwe kidogo inaenda juu kidogo lakini it is a very good way ku-balance-sha mauzo ya nje na imports, kwa sababu imports ikiwa rahisi sana, basi inakuwa kila mtu anataka tu import malighafi. Una-import kwa sababu exchange rate iko very low.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme hivi, kuna issue ya mazingira rafiki ya uwekezaji ya especially kwa private sector; na nataka kumshukuru Mheshimiwa Waziri wa Fedha, ameona umuhimu wa kusema kwamba hakuna kupandisha tozo kwa mamlaka na mamlaka zile zinazohusika na regulations na ya udhibiti wa sekta hizo bila idhini yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, zile zilizopo zipo, lakini amesema sasa kama unataka kubadilisha chochote lazima aione, nami nafikiri hicho ndicho kitu ambacho wadau walikuwa wanalia sana walipokuwa wanakuja kutuona. Wanasema tufanyaje? Hawa wanaweza wakaja tu vilevile, nchi inaweza ikaja ikaingiza, ikapandisha, ikaleta left right na bila kujali viwango, kwa hiyo kuzuia sana watu kupata motisha ya kuwekeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye jambo lingine ambalo ningetaka kutoa ushauri ni kwamba ukiangalia deni la Taifa malipo ya debt services yetu inatisha kidogo, lakini tuko wahimilivu bado kwenye deni, na tunapongeza hilo, lakini kuna jambo ambalo wale wachambuzi walidanganya kwa sababu utakuta tunakopa shilingi trilioni 15 kwenye mpango wa mwaka huu, lakini tunalipa shilingi trilioni 14.2 kama debt services.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, net ni only point eighty of trillion, ni kidogo sana. Sasa unasema ni kitu; naomba Mheshimiwa Waziri wa Fedha aangalie kile kitengo cha Debt Management waone tunafanyaje? Kwa sababu is a lot, huwezi kukopa ili ulipe. Virtually siku utakayokosa mkopeshaji uta-default na/au utapunguza sana matumizi mengine ya maendeleo. Kwa hiyo, hilo ni jambo ambalo nimeliona, nikasema niliseme tu hapa hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ambalo tunapongeza sana ni kwenye sekta ya kijamii, na ninaamini kwamba, ukiangalia kwa mfano sekta ya afya; ndani ya miaka mitano bajeti ya sekta ya Afya imekua kwa 57%, bajeti ya elimu imekua kwa 57% hiyo hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, unaona kwamba kweli kuna jitihada ambazo zinaenda moja kwa moja kumgusa mwananchi, na inachangia sana kwenye masuala ambayo walizungumza akina Mheshimiwa Nahodha, Mheshimiwa Muhongo na hata Mheshimiwa Manya. Kwa hiyo, nafikiri hili ni jambo la kupongeza sana, nami nafikiri kwamba tukiendelea kuzilea vizuri itakuwa ni vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia uone jinsi ambavyo Mheshimiwa Rais anayejali mazingira, bajeti ya mazingira ilikuwa twenty billion, sasa hivi ni sixty-two billion. Kwa hiyo, imekua kwa 210%, ni almost zaidi ya mara mbili. Kwa hiyo, tuwashukuru sana hawa kwa sababu ni jambo ambalo kwa dunia nzima lazima wapongezwe na Serikali yetu ipongezwe kwa sababu tunajali kitu ambacho kinachangia maendeleo na uhimilivu wa dunia yetu kwenda mbele kwa kutunza mazingira. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme tu kwamba pamoja na mengine ambayo yamezungumzwa na wenzangu, naomba niwasilishe na niseme tena kwamba naunga mkono hoja ya Mipango na Bajeti, ahsanteni sana. (Makofi)