Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Same Mashariki
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kwanza nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa zawadi kubwa ya afya na uhai.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninamshukuru sana Waziri, Mheshimiwa Bashe, kila Mbunge atakayesimama hapa atakupongeza na ambaye hatofanya hivyo anakunyima haki yako, unastahili kupongezwa. Mtu akikuangalia haraka haraka anaweza asikufahamu, lakini wewe ni Waziri mzuri sana. Waziri ambaye ni msikivu sana, anayesikiliza Wabunge, anayeshirikiana na wenzie, kubwa kuliko yote yeye ni mchapakazi sana, hongera. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba niongee kwa nguvu kubwa, ninaomba na Watanzania wanisikilize vizuri. Watanzania wenzangu nchi isiyokuwa na chakula inapoteza usalama, nchi ikikosa chakula inapoteza utulivu, sasa mimi ninaomba nitumie nafasi yangu na Watanzania wanielewe kidogo.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ya Awamu ya Sita imefanya jambo kubwa sana, kwa sababu gani ninasema hivyo? Rais - Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani tarehe 19 Machi, 2021 alikuta bajeti ya kilimo ya mwaka 2021/2022 ilikuwa shilingi bilioni 294. Ninaomba Watanzania mpasikilize hapa, alikuta bajeti ya kilimo mwaka 2021 na mwaka 2022 shilingi bilioni 294. Leo hii bajeti ya kilimo yam waka 2025/2026 Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu ameipandisha mpaka imefika shilingi 1,242,000,000,000. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tafsiri ya hilo jambo lililofanywa na Serikali ya Awamu Sita ni pana mno. Siwezi kusimama nikaliongea wala hakuna mtu anaweza akaliongea. Uitoe nchi kwenye shilingi bilioni 294 bajeti ya kilimo uipeleke kwenye shilingi trilioni 1.242. Kwanza ni kwamba amehakikisha kuna utoshelevu wa chakula (food security) kwenye nchi yake, hilo ni la kwanza. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pili, amesimama imara kuhakikisha nchi yake inakuwa na usalama kwa sababu wananchi wakiwa na njaa ndugu zangu ndipo kelele zinapokuwa nyingi. Kwa hiyo, ninaomba Watanzania waelewe kwamba alilolifanya Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali yake, halijawahi kufanywa, ni kubwa mno. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi mimi niseme ukweli mimi ni Mbunge wa Same Mashariki, Jimbo la Same Mashariki 100% liko vijijini. Jimbo la Same Mashariki 100% wanalima, ni kilimo, sasa ukishafanya hivi kwa Jimbo la Same Mashariki hivi mnategemea kweli Samia akapate kura 60% Same Mashariki? Haiwezekani. Wananchi wamemkubali sana, jinsi ambavyo Rais ameamua kukishika kilimo cha nchi hii, hakuna nchi yoyote Afrika Mashariki imefanya hivyo, hakuna. Sisi sasa hivi utoshelevu wa kilimo ni asilimia ngapi? Ni 128%. Nikiwa na maana kwamba sisi tunawauzia majirani zetu hapa, nchi haina kelele. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa mimi ningeomba kuzungumzia jimbo langu kidogo. Ninaomba niongelee jimbo langu; kwanza niipongeze Serikali sana kwamba imejitahidi sana kuhakikisha miundombinu ya kilimo kwenye Jimbo la Same Mashariki inakuwa vizuri sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nianze na Skimu ya Ndungu, mimi kwenye jimbo langu nina skimu ya kisasa moja kubwa ambayo ni ya Serikali inaitwa Skimu ya Ndungu. Ndungu ni kata ambayo ina wakulima zaidi ya 3,000 lakini ile skimu inategemewa na wananchi zaidi ya 16,000. Ninaishukuru Serikali, imekuwa inaingalia ile skimu vizuri sana, ninawapongeza sana. Mheshimiwa Waziri sasa ombi langu kwako, ninaomba Skimu ya Ndungu iangaliwe vizuri zaidi, ninaomba muongeze pesa ili kupeleka kwenye skimu ile kwa sababu wanaoitegemea ni zaidi ya wananchi 16,000. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, niipongeze Serikali, ninaomba nikubali kwamba Serikali iliniletea shilingi bilioni 1.7 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya kilimo katika Kata ya Myamba. Mheshimiwa Waziri lakini nikuombe sasa kazi imefikia 99% lakini bado kuna mifereji mingi ya Kata ya Myamba haijaboreshwa na Kata ya Mpinji hamjaanza kabisa na ndiyo nimeongea na umwagiliaji mkoa wameniambia wameleta request kwako kuomba fedha kwa ajili ya Kata ya Myamba na Mpinji. Ninakuomba ulitekeleze hilo katika mahesabu yako ya hii bajeti ya sasa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba niende kwenye Kata ya Kihurio, haa! Ninaunga mkono hoja. Nimepotezea wapi muda? (Makofi)