Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Azimio la Bunge la Kumthibitisha Waziri Mkuu chini ya Ibara ya 51 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kanuni ya 33 (2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Hon. Prof. Makame Mnyaa Mbarawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkoani

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Azimio la Bunge la Kumthibitisha Waziri Mkuu chini ya Ibara ya 51 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kanuni ya 33 (2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MHE. PROF. MNYAA MAKAME MBARAWA: Mheshimiwa Spika, kwanza ninapenda kushukuru sana kwa kunipa fursa hii kuongea machache kuhusu hoja iliyoko mbele yetu.

Mheshimiwa Spika, ninaomba kumpongeza sana Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ushindi mkubwa na ushindi wa kishindo. Pia, ninapenda kuchukua nafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa Dkt. Nchimbi kwa heshima kubwa aliyopata kuwa Makamu wa Rais wa nchi yetu. Nami ninapenda nichangie hoja iliyoko mbele yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi mwenyewe ninamfahamu sana Mheshimiwa Dkt. Mwigulu. Nina bahati sana kufanya kazi na Waheshimiwa Mawaziri wa Fedha kama wanne katika maisha yangu au katika utumishi wangu wa Wizara, lakini Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ni Mheshimiwa wa kipekee. Nimemwambia Mheshimiwa Dkt. Mwigulu zaidi ya mara mbili kwamba, wewe ni Waziri wa Fedha wa kipekee tofauti na Mawaziri wa Fedha wengine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu huyu anafanya maamuzi, whether ni jambo kubwa Mheshimiwa Dkt. Mwigulu anafanya maamuzi. Baadhi ya watu wanachukua muda mrefu kufanya maamuzi, lakini Mheshimiwa Dkt. Mwigulu anafanya maamuzi. Leo hii Waheshimiwa Wabunge na leo hii tunaona miradi mingi mikubwa ya kimkakati inaendelea nchi hii kwa sababu ya usaidizi mkubwa wa Mheshimiwa Dkt. Mwigulu kumsaidia Mheshimiwa Rais. Mheshimiwa Dkt. Mwigulu anafanya kazi kubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tumefanya kazi kubwa sana na Mheshimiwa Dkt. Mwigulu katika kipindi chote, amekuwa na maono makubwa, amekuwa mtafutaji mkubwa kumsaidia Mheshimiwa Rais kutafuta fedha na amekuwa msimamizi mkubwa kwenye miradi mikubwa ya kimaendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambao Waheshimiwa hawajui Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ni mtu mkweli, ni mtu mkweli na anasimamia haki. Mheshimiwa Dkt. Mwigulu hapendi kumwonea mtu. Tumekuwa na incidence nyingi ambazo Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesimama kidete kuwatetea watu wengine. Ninampongeza sana Mheshimiwa Dkt. Mwigulu kwa uteuzi huu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu anapenda haki na Mungu amemjalia leo amekuwa Waziri Mkuu Mteule, tunaamini ataendelea kufanya kama alivyofanya huko zamani. Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kumleta Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba hapa mbele yetu, huyu ni Waziri Mkuu ambaye atatuvusha katika kipindi hiki kwa sababu ana uwezo mkubwa, ana maono makubwa na anapenda kutenda haki, nami ninakushukuru sana na ninaomba sana Waheshimiwa Wabunge kwa pamoja tuunge mkono Azimio lililopo mbele yetu, tuweze kutenda haki kwa Mheshimiwa Rais na Watanzania kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa fursa hii. (Makofi)