Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nikushukuru kunipa nafasi hii nami niweze kuchangia katika mjadala wa hotuba yetu leo na kabla sijaanza nitumie nafasi hii kumshukuru Rais wetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye kimsingi ndiye ambaye ametuamini lakini ndiye anayetoa fedha na anayetoa miongozo yote katika sekta yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie nafasi hii pia kuwashukuru Mheshimiwa Makamu wa Rais, Mheshimiwa Waziri wetu Mkuu, Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu ambao ndiyo viongozi na wasaidizi wakuu wa Mheshimiwa Rais katika kazi yetu hii ya kujenga taifa letu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kipekee pia nitumie nafasi hii kumshukuru Mheshimiwa Waziri wetu mpendwa, Mheshimiwa Profesa Makame Mbarawa Mnyaa ambaye ndiye ambaye anayetuongoza kwenye sekta kwa kutusaidia na kutuongoza wakati wote ili kutimiza malengo ambayo Mheshimiwa Rais ameweza kutukabidhi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie nafasi hiyo pia kumshukuru Katibu Mkuu wa Wizara yetu Mheshimiwa Kahyarara na Naibu wake Mheshimiwa Nduhiye pamoja na watendaji wote, Wakurugenzi Makao Makuu pamoja na Watumishi kwa ujumla, Wakuu wa Taasisi, Wenyeviti wa Bodi pamoja na Wajumbe wa Bodi Mbalimbali ambao kimsingi tunashirikiana nao katika shughuli za kila siku. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nimeona Watumishi wenzetu wako hapa, wahudumu kwenye sekta zetu mbalimbali, wapo wa kwenye ndege, wapo wa kwenye meli, wapo wa kwenye treni. Wote tunawashukuru sana kwa sababu wanatupa ushirikiano mzuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, kipekee pia nitumie nafasi hii kuwashukuru viongozi wenzangu katika wilaya yetu ya Mufindi kwa kutuongoza, Chama Cha Mapinduzi na Serikali lakini Wanaccm wenzangu na Wananchi wa Jimbo la Mufindi Kusini kwa kuendelea kuniamini na kunisaidia katika kutimiza majukumu yangu haya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie nafasi hii pia kushukuru familia yangu kwa kazi ambayo wananisaidia kunivumilia kwenye majukumu ya kila siku. Aidha, Mheshimiwa Spika mwenyewe ambaye ndiye kiongozi wetu akisaidiwa na Naibu Spika na wewe mwenyewe Mheshimiwa Mwenyeti na Wenyeviti wengine kwa kazi kubwa mnayomsaidia katika kuongoza kazi hii pamoja na Kamati yetu ya kisekta na Kamati zingine na Wabunge wote wa Bunge hili kwa kazi ambayo wanaifanya ya kujenga Taifa letu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wachangiaji katika kikao cha leo walikuwa wengi lakini pia siku za huko nyuma tulipokea michango mbalimbali ambayo inagusa sekta yetu. Mheshimiwa Waziri yote kwa umoja wake ameweza kuipokea amejipanga kama sekta kwa ajili ya kufanyia kazi. Nishukuru kipekee waliochangia kwa maandishi na waliochangia moja kwa moja. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, michango ya leo inadhihirisha mambo mengi lakini kwa uchache inadhihirisha umakini na uhimara wa Bunge letu Tukufu la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwamba ni Bunge la vitendo, Bunge la matokeo lakini pia inathibitisha umadhubuti wa CCM kuwa tayari katika kuendelea kuongoza nchi yetu leo, kesho na kesho kutwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia Bunge hili linazidi kudhihirisha kwamba ni Bunge la maslahi ya wananchi. Bunge la matokeo zaidi. Lakini mwisho wa michango hii imepeleka sifa nyingi sana kwa Rais wetu mpendwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye kipekee kupitia anavyotuongoza kwa miaka hii minne ameonyesha kipaji cha uongozi, ameonyesha upekee katika uongozi, ameonyesha maono katika uongozi, utulivu wa hali ya juu hata pale kunapokuwa na kelele nyingi katika nchi yetu. Lakini yeye amekuwa ni mtulivu akiendelea kuchapa kazi zake vizuri, tumuombee Mheshimiwa Rais maisha marefu na afya njema ili aendelee kuipaisha nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu imebahatika kuwa katika nafasi nzuri ya kimkakati na imekuwa ni maombi ya wananchi pamoja na Wabunge mbalimbali hapa wakati wote kwamba tutumie faidi hii ya kuwepo kwetu kimkakati kuweza kulisha au kuhudumia karibu nchi nane ambazo hazina bandari zinatutegemea sisi. Dkt. Samia Suluhu Hassan amedhihirisha hilo amefanya maamuzi mbalimbali ni mashahidi mwaka juzi tu hapa tulipokuwa tunazungumzia habari ya kuongeza wawekezaji binafsi katika sekta yetu ya bandari kulikuwa na kelele nyingi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pamoja na kelele zile maamuzi aliyoyafanya ya kuingiza wawekezaji hawa pamoja na faida nyingine nyingi naweza kuongea mambo makuu mawili. Kwanza kama ilivyozungumzwa na wenzangu ni kuongezeka kwa fedha za kikodi, mapato ya kikodi karibu trilioni 1.2 ambayo kutoka 7.08 mpaka kufikia 8.2 ngapi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ukiacha hiyo imeongezeka pia gharama za matumizi kwenye bandari za uendeshaji zimeshuka kwa takribani bilioni 290, ukichukua kipengele hiki peke yake unaona karibu trilioni 1.5 imeweze kutengenezwa katika mwaka huu mmoja. Ndiyo maana napata ujasiri sasa wa kuongeza mishahara ya wafanyakazi, anapata ujasiri sasa wa kuongeza fedha kwenye barabara, anapata ujasiri sasa wa kupeleka fedha kwenye maji huu ni utulivu na umakini wa hali ya juu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na jambo hilo kubwa ambalo limefanyika Dkt. Samia Suluhu Hassan ameamua kubadili hii Sekta ya Uchukuzi kwa kufanya maboresho katika maziwa makuu. Limezungumzwa hoja ya kwanza hapa namna ya kuongeza usafirishaji kwenye upande wa bahari. Baharini tayari alishatoa maelekezo tumeishampata mkandarasi hivi ninavyozungumza anafanya usanifu kutazama biashara iliyopo katika ukanda wa bahari yetu pamoja na maeneo jirani kama kina Visiwa vya Comoro na maeneo mengine. Itakapokamilika katika mwaka wa fedha utakaofuatia tutaanza maandalizi kwa ajili ya kujenga meli hizo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pili katika maziwa makuu amezungumza Mheshimiwa Kilumbe pale Dkt. Samia Suluhu Hassan kazi kubwa aliyoifanya ya kihistoria moja ni kukarabati meli zote zilizopo katika Ziwa Tanganyika. Hivi navyozungumza Meli ya MV Mwongozo tayari Mkandarasi amepatikana, hivi navyozungumza Meli ya Liemba tayari Mkandarasi amepatikana na anajenga yuko asilimia 15. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi navyozungumza MT Sangara ipo asilimia 98 pamoja na hilo tunajenga kiwanda kikubwa cha kujengea meli na kukarabati meli katika Ziwa Tanganyika na hii ni kwa sababu kwenye Ziwa Tanganyika nchi kubwa ambazo zinamiliki ziwa hilo ni Tanzania pamoja na Congo. Maana yake ni nini? Tukiyafanya haya yote usafiri wa reli ya SGR utakaofungamanishwa na bandari ambazo zimejengwa kwenye Ziwa hilo utarahisishwa sana na meli hizi ambazo zinajengwa. Hii ni habari njema sana kwa wenzetu wa Mikoa ya Kigoma, Katavi pamoja na Rukwa kwa namna ambayo itakwenda kuwanufaisha zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini katika kuvutia wawekezaji Serikali imefanyakazi kubwa kuvutia wawekezaji. Ninapozungumza hapa tayari tunaye mkandarasi ambaye anajenga meli nne kwa mkupuo za tani elfu mbili mbili na inategemewa ndani ya miaka miwili kuanzia tarehe 01Aprili, 2025 zitakuwa zimekamilika. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi yake itakuwa ni kuchukua madini kutoka Kalemi ambako bandari inajengwa kuja mpaka bandari zetu na kisha zitasafirishwa kwenda mpaka Dar es Salaam na mwaka wa kwanza tutakuwa na almost tani laki sita, maboresho haya yanakwenda sambamba kwenye maziwa, Ziwa Victoria, Ziwa Nyasa na maeneo mengine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelezo hayo naomba kuunga mkono hoja. (Makofi)