Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Uchukuzi kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

Hon. Mwantumu Mzamili Zodo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Uchukuzi kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

MHE. MWANTUMU M. ZODO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nachukua fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa aliyoifanya kwenye Taifa letu kuhakikisha anatutoa sehemu moja kutupeleka sehemu nyingine.

Pia tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuendelea kuboresha viwanja vya ndege na usafiri wa anga kwa ujumla, kuendelea kuboresha vivuko pamoja na usafiri wa reli kwa ujenzi wa reli ya kisasa ambayo inakwenda kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza sana Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri pamoja na watendaji wote wa Wizara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali yangu tukufu na sikivu kuendelea kuboresha viwanja vyetu vya ndege kikiwemo kiwanja cha ndege cha Tanga.

Pia naiomba Serikali kuendelea kuboresha vivuko vyetu hasa kivuko chetu cha Pagani, kivuko hiki kina changamoto kubwa na kinasababisha adha kubwa na kuhatarisha maisha ya wananchi wetu. Kivuko hiki mpaka sasa hakifanyi kazi, imekuwa changamoto sana kwa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo naunga mkono hoja.