Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. ZULFA MMAKA OMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kumshukuru Allah kwa kutujalia uzima na kuweza kuchangia leo hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa ya kuijenga nchi yetu. Hakika ni Rais mwenye maono ya mbali. Pia nimpongeze Waziri na Naibu Waziri wake kwa jinsi wanavyoiongoza Wizara kwa umakini mkubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu nitajikita kwenye reli ya kisasa za SGR. Naamini reli hii imekuja kutatua shida za usafiri kwa Watanzania. Ila kuna shida pale unaposafiri na kamzigo chako cha zawadi kama vile korosho, ubuyu na vitafunwa vingine ambavyo sisi Watanzania tuna utamaduni wa kupelekeana zawadi. Ila kwa upande wa stesheni wanalazimisha uviache pale kwa sababu hairuhusiwi kubeba chakula.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe muweke utaratibu maalum ili tuweze kubeba zawadi zetu, kwani kuna wanafunzi pia wanapotoka majumbani kuelekea boarding wanabeba chakula chao yaani vitafunwa kwa ajili ya kuwasaidia siku kadhaa, ila wanapofika stesheni wanaambiwa hairuhusiwi kubeba. Naomba hili liangaliwe kwa huruma sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.