Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. AMINA ALI MZEE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi hii, kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia uhai na uzima nami kupata nafasi hii ya kuchangia Bajeti hii ya Wizara ya Uchukuzi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nitumie nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Mheshimiwa Naibu Waziri pamoja na Watendaji wote wa Sekta ya Uchukuzi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie nafasi hii kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mapinduzi makubwa ambayo ameyaleta ndani ya sekta hii ya uchukuzi. Leo hii Tanzania tunajionea, tuna reli, tuna ndege, tuna meli, Daktari Samia ndio ambaye amezileta. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mapinduzi haya makubwa katika sekta ya uchukuzi Daktari Samia amedhamiria dhahiri kuhakikisha Tanzania inaendelea ndani ya sekta ya uchukuzi. Tuna kila hatua ya kuhakikisha Daktari Samia tunamrudisha tena katika urais 2025. Nimpongeze sana Daktari Samia kwa kuendelea kuhakikisha sekta ya uchukuzi inaendelea kupiga hatua katika nchi hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nijikite katika mchango wangu. Sekta ya Uchukuzi ina vyuo mbalimbali. Vyuo ambavyo vinazalisha elimu na ujuzi mbalimbali kwa vijana wetu. Ndani ya sekta hii ya uchukuzi kuna Chuo cha NIT, Chuo cha DMI, Chuo cha Usafirishaji, vyuo vyote hivi vinazalisha nguvu kazi ya Taifa hili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna Chuo cha Usafirishaji, Serikali imeeleza ndani ya bajeti hii juu ya ununuzi wa flight simulator kwa ajili ya wananfunzi. Flight simulator hii itakwenda kuchochea, kukuza uelewa wa wanafunzi wetu ambao wanazalishwa ndani ya Chuo cha Usafirishaji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie nafasi hii Mheshimiwa Waziri, Mheshimiwa Naibu Waziri na Watendaji ambao wapo ndani ya sekta ya uchukuzi mchukue tahadhari na jitihada za makusudi kuhakikisha mnakwenda kutoa elimu juu ya uzalishaji wa marubani katika Taifa hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona na mmeeleza juu ya uchache wa Marubani ambao wapo ndani ya Taifa hili. Twende tukatumie vifaa ambavyo vimeletwa ili kuhakikisha tunazalisha Marubani wanaoweza kuendesha ndege ambazo Rais wetu ameendelea kuzinunua ndani ya Taifa hili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna Chuo cha Reli. Tuna reli ambayo inaendelea ya SGR. Reli yetu ya SGR inahitaji ujuzi na uelewa na ufanisi mkubwa. Teknolojia inayotakiwa kuendeshwa ndani ya reli hii ni ya hali ya juu, tuendelee kutoa elimu kwa vijana wetu juu ya matumizi mazuri ya reli, uendeshaji pia utunzaji wa miundombinu ya reli. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, reli yetu Serikali imetumia fedha kubwa kuhakikisha reli inaijengwa. Kwa hiyo, kwa makusudi tuhakikishe reli hii inajengwa lakini inatunzwa, vipi itatunzwa na vipi itatunzwa na vipi itaendelezwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, elimu kubwa inahitajika kuwekezwa kwa Chuo chetu cha Reli kuhakikisha wanawapa training ya kutosha juu ya ujenzi wa miundombinu ya reli, vichwa vya treni pia uharibifu utakapotokea jinsi gani hatua za haraka za kuhakikisha wanaweza kutengeneza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie nafasi hii kuhakikisha jinsi gani wanaweza kuendeleza ujenzi wa meli. Tuna ujenzi ambao unaendelea wa meli ndani ya Maziwa Makuu. lakini tuchukue jitihada za makusudi kuwawezesha vijana, kuwajengea elimu juu ya kuweza kutengeneza meli hizo. Meli zitakuwepo na zitaendelea kubakia, wataalam wataondoka. Tuhakikishe wataalam ambao wamekuja kutengeneza meli zile wanawapa knowledge ya kutosha vijana wetu ili waweze kuhakikisha wakiondoka knowledge ile itaendelea kubakia na kuliendeleza Taifa letu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie nafasi hii kuipongeza Serikali inayoongozwa na Daktari Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuleta maendeleo ndani ya sekta hii ya uchukuzi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sina mengi naomba kuunga mkono hoja. (Makofi)