Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Iringa Mjini
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, ninapenda kuchukua fursa kuwapongeza Wizara kwa mambo mengi mazuri waliyofanya. Hata hivyo, ninaomba mambo haya yafanyiwe kazi.
Mheshimiwa Naibu Spika, moja ni suala la NHC kudai key deposit kwa wapangaji wa zamani sasa, kwa rate ya sasa na siyo ya upangaji wao walipoingia, siyo sawa kisheria. Jambo hili linaleta malalamiko mengi kwa wapangaji ambao ni wananchi. Utaratibu kwa mujibu wa mikataba yao unahitaji watoe key deposit kabla ya kuingia katika nyumba hizo na inatakiwa itozwe kwa wapangaji wapya. Sasa hii ya kuwatoza wapangaji wa zamani kwa uzembe uliofanywa na shirika lenyewe kutodai au kupoteza kumbukumbu za wateja, sio sawa.
Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuondoa usumbufu wa migogoro isiyokuwa ya lazima kwa kushtakiwa na wapangaji na kuliingizia shirika hasara zisizo za msingi, basi utaratibu ufuatwe kwa wapangaji wapya na wale wa zamani watozwe kwa kodi waliyoingilia kwenye majengo hayo, iwapo watajiridhisha kuwa haikutolewa. Siyo kwamba, hawaoni kumbukumbu yoyote au wawaache, ila warekebishe kwa wapya.
Mheshimiwa Naibu Spika, kama issue ni hoja ya CAG, wamwambie kwa sasa wamerekebisha, ndiyo maana amewekwa Mkurugenzi mpya, ili arekebishe. Siyo tena kuharibu zaidi kwa kukiuka taratibu na kuleta migogoro isiyo ya lazima. Mimi pia, ni mpangaji humo, nina uhakika na ninachokisema.
Mheshimiwa Naibu Spika, pili. Upandishaji wa kodi uzingatie pia, ukuaji wa uchumi wa Taifa, ili kuendelea kuzingatia hasa lengo la uanzishaji wa Shirika la NHC. Siyo kushindana kwenye soko tu, bali kusaidia kupatikana kwa makazi ya bei nafuu.
Mheshimiwa Naibu Spika, tatu, utatuzi wa migogoro ya ardhi. Tunaomba sana utaratibu madhubuti wa kutatua migogoro ya ardhi, uwekewe mpango mahususi wa kutatua migogoro hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kipekee katika Mkoa wa Dodoma, tunaomba migogoro itatuliwe, ili iwe kweli, fahari ya Watanzania kwa kujengwa kwake kwa wakati. Tunadai viwanja vilivyofanyiwa double allocation kwa zaidi ya miaka mitano sasa na wengine zaidi ya hapo, sasa hii siyo sawa!
Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri sasa; kama Wizara wameshindwa kutatua migogoro ya ardhi Dodoma, basi iundwe tume maalum ishughulikie suala hilo, kama ilivyokuwa Tume ya Jiji au Tume ya Keenja, maana kliniki zimekuwa nyingi, lakini matatizo hayaishi.
Mheshimiwa Naibu Spika, nne; Mipango Miji waandae mipango miji kwa eneo lao lote la utawala, siyo kwa vipande vipande. Hii inasababisha ujenzi holela katika miji. Kwa kuwa, wanaanza kupanga huku, upande mwingine unavamiwa. Ule utaratibu wa vijiji vya ujamaa uangaliwe, ili kupunguza ujenzi holela na kufikisha huduma za jamii kirahisi zaidi. Tutapunguza gharama kubwa ya kupeleka miundombinu kwa gharama kubwa kwa wananchi wachache.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kuwasilisha.