Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

Hon. Jesca Jonathani Msambatavangu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Iringa Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Ninashukuru kwa kunipa nafasi, nilipata udhuru kidogo. Mengine nimeyaweka kwa maandishi, lakini nitakuwa na machache tu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nawapongeza Wizara ya Ardhi kwa kazi kubwa wanayoifanya, lakini ombi langu la kwanza Mheshimiwa Waziri ni NHC. Kuna utaratibu umekuja sasa hivi kwamba, mna-charge key deposit; sasa unakuta mna wapangaji, wale ambao walishapanga muda mrefu, halafu mmewaletea demand walipie key deposit, mtu ameshakaa miaka minne, mitano, unamdai sasa hivi alipe key deposit! Wakati ile key deposit ilikuwa ni kodi ya mwanzo kabla hajaingia, unam-charge miezi mitatu, analipa, then analipa kodi yake anaendelea. Sasa ni kinyume cha utaratibu na wananchi wanalalamika, tunaomba Mheshimiwa Waziri hilo akalifanyie kazi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kingine, amesema hapa, tuwe na affordable houses. Tunaomba kabisa Mheshimiwa Waziri hizi nyumba za National Housing kodi zao wasizingatie tu market, turudi kule tulipoanzisha shirika tulikuwa na nia gani. Waangalie na jinsi uchumi wa nchi unavyokwenda bila kuangalia tu market ya eneo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kingine, ninaomba sana Mheshimiwa Waziri katika kupanga hii miji watusaidie, wasipange miji kwa vipandevipande, kila watu kwenye mamlaka yao waupange mji mzima. Kwa mfano, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wawe na masterplan ya halmashauri yote, wasianze kata hii kata hii; wanapoanza kata hii, kule kata nyingine kumevamiwa. Kwa hiyo, tunaomba kila sehemu yenu ya Idara ya Ardhi, kwenye eneo lao la utawala, wawe na masterplan ya eneo lote, ili kuzuia kule mbele kusivamiwe. Wakiweza warejee ile Sheria ya Vijiji vya Ujamaa tulivyokuwa tunafanya sogeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, nia ilikuwa ni kusogeza huduma karibu na wananchi, kuwaweka wananchi pamoja, iwe rahisi kuwahudumia. Leo hii tunalazimika kupeleka umeme sehemu nyingine kwa gharama kubwa kwa sababu tu, hatuku-plan ule mji watu wakakae kule. Wakishafika kule watakudai maji, watakudai umeme, watakudai barabara, bajeti ya jimbo zima unakuta inaelekea kwenye kijiji kimoja ambacho watu walienda kuishi mashambani. Sasa watusaidie kupanga hii miji.

Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho ni suala la Dodoma, ni fahari ya Watanzania. Dodoma ni fahari ya Watanzania, lakini siyo fahari ya migogoro ya ardhi kwa Watanzania. Hakuna Jiji lina migogoro ya ardhi kama hili la Dodoma. Ninaomba sana, Mheshimiwa Waziri alifanyie kazi, sijui watafanyaje?

Mheshimiwa Naibu Spika, kama wanadhani kwamba, imeshindikana kwa utaratibu wa kawaida wa ardhi, basi iundwe tume kama, zile za akina Keenja, kama inashindikana basi hizo kamisheni watengeneze. Kwa kweli, watu wa Dodoma wamekuwa loyal kwa Serikali hii na Serikali zote za Chama Cha Mapinduzi, lakini namna ambavyo tunabanana nao, kila siku wanaandamana kwenye Ofisi za Mipango Miji, inasikitisha sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, wazee wanalalamika. Unakuta akinamama wanalia mle. Mimi mwenyewe, Mbunge, nimefanyiwa double allocation Dodoma, wapo wengi tu humu. Walikuja wakatuuzia viwanja kwenye kliniki, kumbe viwanja hewa! Tumepata double allocation, kila siku tunapanga foleni, huu ni mwaka wa tano tunakwenda kumaliza Ubunge hatujawahi kupewa viwanja vyetu. Sasa hawa Watanzania wengine na hii fahari yetu iko wapi, Mheshimiwa Waziri?

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba iwe fahari yetu, lakini tusinune. Tuujenge mji kwa haraka. (Makofi)

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Naibu Spika, Taarifa.

TAARIFA

NAIBU SPIKA: Taarifa.

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Ninataka nimpe Taarifa dada yangu, Mheshimiwa Jesca Msambatavangu, kwa mchango wake mzuri anaochangia kwamba, ni kweli kabisa kumekuwa na ukiritimba kwenye Ofisi za Ardhi. Mimi mwenyewe hapa nina zaidi ya miezi nane ninasubiri control number, ninaambiwa mtandao haufanyi kazi.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa, kaa inatosha.

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

NAIBU SPIKA: Inatosha. Mheshimiwa Jesca, Taarifa hiyo?

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, ninapokea Taarifa yake na ninaomba sana, tunataka Dodoma iendelee kuwa fahari yetu, lakini wapunguze migogoro ya ardhi, Wanadodoma wasione kama sisi wageni tumekuja kuwapora. Sisi wageni watukaribishe kwa wema, watupatie viwanja. Kliniki tunaingia na magonjwa, tunatoka na magonjwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaunga mkono hoja. (Makofi)