Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arumeru-Magharibi
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. NOAH L. S. MOLLEL: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia Bajeti ya Wizara ya Ujenzi. Nianze kwa kumshukuru sana Mungu kwa kunipa nguvu na afya ya kuwepo katika Bunge hili kwa siku ya leo na hata siku zingine zilizopita.
Mheshimiwa Naibu Spika, hotuba yangu itajikita zaidi kwenye yaliyotekelezwa lakini pia yale ambayo tunaomba Wizara hii iweze kutusaidia kukamilisha na nyingine kutekeleza. Nianze pia kwa kumshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jinsi ambavyo anaendelea kutuhudumia kwa nyanja zote afya, maji, barabara na kadhalika.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimshukuru pia Mheshimiwa Waziri wetu Mheshimiwa Ulega pamoja na Mheshimiwa Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu na watumishi wote wa Wizara kwa jinsi ambavyo wanajitahidi kuhakikisha kwamba tunakwenda vizuri kwenye ujenzi wa barabara.
Mheshimiwa Naibu Spika, niendelee kwa kusema kwamba ninaanza na shukrani kwa Rais na Wizara kwa maana ya Mheshimiwa Ulega, mwenyewe kwa kukamilisha fidia ya wananchi wa Barabara ya Mianzini - Sambasha kuja Ngaramtoni kiasi cha shilingi bilioni 3.5. Kwa niaba ya hao wananchi tunashukuru sana Serikali ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutoa fidia hiyo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, hatutoi shukrani kwa maana ya ujenzi wa barabara hiyo unaendelea mkandarasi yupo kazini na mpaka sasa mkandarasi ameshalipwa zaidi ya bilioni 8.1, tunatoa shukrani nyingi sana kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Arumeru Magharibi.
Mheshimiwa Naibu Spika, ombi langu kwa Mheshimiwa Waziri, tunaomba kwamba mkandarasi yupo kazini, lakini bado anasuasua kwa sababu ile flow ya pesa ni kidogo. Kwa hiyo, ninaomba sasa kumwomba kwa heshima kubwa Mheshimiwa Waziri na amekuja kwenye barabara hiyo tukazungumza kwa kweli tunakushukuru kwa msukumo wake, maana alipokuja alitupatia tena fedha kidogo mkandarasi akasogea.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nimwombe kwa heshima kubwa tunaomba sana barabara hiyo kwa sababu tunaelekea huko tunapoelekea basi tuangalie angalau kabla ya kipindi hiki uweze kurusha hela kidogo, mkandarasi aendelee kwa kasi kubwa ili tuone wananchi wetu wanafurahia barabara hiyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba pia mkandarasi huyo anaendelea vizuri kufanya kazi na Meneja wetu wa mkoa anafanya kazi nzuri sana kwa kweli kitu ambacho anatusaidia pale ambapo tunapata changamoto hasa katika mambo ya mafuriko, mambo ya nini anatusaidia sana Meneja wetu wa Mkoa. Mheshimiwa Waziri tunaomba barabara hiyo sasa kama ambavyo alikuja tukamwomba isiishie kule forest kwa sababu ikiishia forest itakuwa haileti maana kamili.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba lile ombi ambalo tumemwomba mbele ya wananchi na Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa akamwomba, Mheshimiwa Mwenyekiti wetu wa Mkoa wa CCM akamwomba, basi ninaomba hilo alichukulie kwa uzito wa aina yake kwa sababu itapata maana kubwa sana pale ambapo itakuwa imekuja kuunganisha kwenye Chuo chetu cha Forest inayoenda Golomotonyi inakuja kuungana na Barabara ya Nemanga itakuwa imetusaidia sana katika kuleta maana halisi kwenye barabara hiyo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna suala la mafuriko ambalo inakuja kuathiri Barabara ya bypass Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa na RAS wameunda Kamati ya Wataalamu wakiwemo TANROADS na taasisi zingine kwa ajili ya kuhakikisha kwamba wanaenda kuangalia mafuriko hayo ambayo inakuja kukata hiyo barabara ya bypass.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nimwombe ripoti hiyo itakapokamilika na kuwasilishwa basi achukulie kwa uzito wa aina yake kwa sababu barabara hiyo inakwenda kubomoka na inaweza ikakatika. Ni barabara ambayo imetengenezwa kwa pesa nyingi zaidi kwa sababu usipoziba ufa utajenga ukuta. Nimwombe sana na anajua barabara ni siasa na siasa ni Barabara. Kwa hiyo, ninaomba hilo alichukulie kwa aina yake.
Mheshimiwa Naibu Spika, niende kwenye Barabara ya Arusha – Simanjiro – Kongwa kuja Dodoma, tunashukuru sana Serikali kwa sababu mmesaini mkataba wa kilomita 70 ambayo ni sawa na bilioni karibu 221,350,265,000, tunashukuru sana. Tunaiomba basi Serikali mkandarasi huyo kwa sababu amesaini mkataba ile mwezi wa pili, niombe sana mkandarasi huyo aingie kazini. Ili yale malengo yetu ya kujenga barabara hiyo. Kwa sababu kwenye jimbo langu nina kilomita 28 kutoka T. Packers School kuja Losonyai.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna ule upande wa Mbauda kilomita 22, kwa hiyo, jumla kwa upande wetu sisi tuna kilomita 50 ikienda tena mbele itakwenda kwenye Jimbo la Simanjiro ambayo nayo wataendelea na hizo kilomita zingine hadi kufika huku Dodoma. Kwa hiyo, naomba sana kuishukuru Serikali na nimwombe mkandarasi huyo aweze kuingia. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ombi lingine tunaomba pia wakati wa ujenzi wa hizi barabara basi viwekwe vibanda vya bodaboda kwa sababu wana-park kila mahali bila utaratibu tunaomba sana hili nalo ni muhimu katika hilo.
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, kwa sababu ya muda ninaomba kuunga mkono hoja, lakini yote haya ambayo yamepangwa basi yakatekelezwe chini ya Waziri wetu Mheshimiwa Ulega. Ahsante sana. (Makofi)