Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Gairo
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. AHMED M. SHABIBY: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuwa mmoja wa wachangiaji dakika ni chache tutakwenda kidogo haraka haraka. Kwanza nimpongeze Mheshimiwa Waziri, Mheshimiwa Naibu Waziri pamoja na Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Mtendaji Mkuu wa TANROADS na timu yote ya TANROADS maana yake usipokuwa unasema ukweli unakuwa ni mchawi au mnafiki, kwenye ukweli lazima tuseme ukweli, kwamba TANROADS wanajitahidi sana lazima tuwapongeze na tuwape moyo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na hizi pongezi tatizo linalokwamisha TANROADS ni pesa na lazima tuangalie pesa ndiyo kikwazo kikubwa kwa TANROADS lakini kila siku zinavyozidi kwenda barabara zinazidi kuongezeka. Kwa hiyo, changamoto kwenye TANROADS lazima ziwepo na barabara za zamani nazo zinachakaa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano, kama hii ya Morogoro – Dodoma sasa hivi muda wake ule wa kutengenezwa umeshafika lazima itengenezwe tena upya barabara nyingine ni mpya. Kwa hiyo, lazima tutafute chanzo Mheshimiwa Waziri lazima watafute chanzo kingine wapendekeze kwenye Kamati ya Bajeti wapate vyanzo mbadala kwa ajili ya kuweza kuisaidia TANROADS ipate pesa ili Waheshimiwa Wabunge wote tufurahi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia kwenye upande wangu wa Jimbo langu la Gairo Mkoa wa Morogoro na ukiangalia Wilaya ya Kilindi Mkoa wa Tanga kuna barabara moja muhimu sana tumekuwa mimi na Mheshimiwa Mbunge wa Kilindi Mheshimiwa Omari Kigua tunaifuatilia kwa karibu sana barabara hii. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nawaomba watu wa TANROADS safari hii niwapongeze wametujengea madaraja makubwa sana ambayo katika historia ya ile barabara. Hata hivyo, pale Matare panahitaji makaravati tu makubwa ili barabara ile yote iweze kupitika kuanzia Gairo mpaka Kilindi na mwaka huu ninajua wameweka kwenye feasibility study kwa ajili ya kujenga kwa kiwango cha lami. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ile Barabara ukitoka Tanga kupitia Handeni – Kilindi - Gairo - Dodoma ni karibu sana kuliko barabara nyingine yoyote kwa kutokea Dodoma. Tunaomba Mheshimiwa Waziri, aifuatilie sana hii barabara na Mheshimiwa Naibu Waziri alipita na Mheshimiwa Waziri alipita wakasema kweli barabara hii ni nyepesi, tunaomba kwenye feasibility study ifanyike waitafutie pesa ziwekwe pale. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pale kwenye kipande kile cha Gairo – Nongwe, ile feasibility study ninafikiri imeshakwisha, tunaomba waitengee sasa pesa kwa ajili ya kutengenezwa kwa kiwango cha lami. Pale Gairo Mjini alishapewa mkandarasi ninafikiri kama kilomita moja hivi kwenda mpaka hospitali ya wilaya, lakini ndiyo hiyo Barabara ya Nongwe alichimba chimba akapachafua lile eneo ameliacha kama ilivyo. Tunaomba tujue huyu mkandarasi kuna tatizo gani eneo lile? Ili aweze kumaliza kile kipande cha ile barabara. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile kuna yale maeneo ya milima maana yake tunaposema Nongwe milima yake ni mikubwa kuliko hata ile milima ya kwenda Lushoto. Kuna wale wakandarasi ambao wamewapa pale kwa ajili ya kuweka zege maeneo ya milimani toka mwaka juzi mpaka mwaka huu unaona bado wanasuasua magari mengi yanapata matatizo yanaanguka watu wenye pikipiki wanaanguka, wenye magari makubwa yanaanguka.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunaomba wafuatilie. Kwa vile dakika ni chache naomba niwashukuru sana Wizara ya Ujenzi, wanafanya kazi nzuri, hongera sana. Ninaunga mkono hoja na ahsante sana. (Makofi)