Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa nafasi ya kuchangia. Awali ya yote ninamshukuru Mwenyezi Mungu mwenye enzi na utukufu kwa kuniwezesha kusimama katika Bunge hili kwa muda na wakati kama huu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ninachukua fursa hii pia kuipongeza Serikali inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa inayofanya ya kuhakikisha Taifa letu linaendelea kuunganika kwa kupitia mtandao wa barabara na nchi za Jirani; pia, mikoa yetu na wilaya zetu zinaweza kuunganika. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaipongeza sana Serikali kwa kazi kubwa inayofanya licha ya changamoto kubwa ya mabadiliko ya tabianchi. Tumeona jitihada kubwa za Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha anakwenda sambamba na changamoto hiyo. Hivi juzi tumesikia ameongeza shilingi bilioni 30 ili kuweza kutatua changamoto zinazotokea kutokana na mabadiliko ya tabianchi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ninachukua fursa hii pia kuwapongeza watendaji wa Wizara wakiongozwa na Mheshimiwa Ulega, mtu bingwa kabisa. Nimeiona speed yake namna ambavyo aliwatia pin wale jamaa ambao walifungua kila sehemu ya Barabara ya Dar es Salaam halafu wakawa hawaeleweki. Nimependa ile initiative; anatenda kwa haraka na matokeo yanatokea kwa haraka. Hongera sana kwa Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu wake pale, mtu bingwa kabisa, Mzee wa busara Engineer Kasekenya mwenyewe, watendaji wa Wizara pamoja na taasisi zake. Ninachukua fursa hii kuwapongeza kwa kazi kubwa wanayofanya. Hakika tukiiangalia TANROADS iliyoanzishwa mwaka 2000 na kazi kubwa ambayo imefanya sasa hivi kwa Taifa letu licha ya changamoto ndogondogo zilizopo, ninasema TANROADS wanaupiga mwingi sana. Taifa letu linapata connectivity na watu wanaweza ku-access kutoka sehemu moja na sehemu nyingine. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kipekee kabisa ninampongeza Mheshimiwa Engineer Mohamed Besta kwa kazi nzuri anazofanya. Mimi ninasema, wakati nikiwa junior engineer pale Wizara ya Ujenzi, ninakumbuka kabisa nilikuwa ninasoma pavement material design manual nikiona jina la Mhandisi Besta pale. Kwa hiyo, ni mtu mwenye profession yake anayoimudu. Tuendelee kumpa maua yake ili atusaidie kuiongoza TANROADS yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kusema kwamba Mheshimiwa Waziri ametaja vipaumbele vya bajeti yake na moja wapo ya kipaumbele amesema kwamba bajeti hii itakwenda kutekeleza miradi ya mkakati na miradi ambayo inakwenda kufungua fursa za kiuchumi pamoja na kuondoa msongamano nchini. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pale Mkoa wa Tanga tuna barabara ambayo economic potential yake ni kubwa mno kwa Taifa hili. Barabara inayounganisha Makutano ya Kiomoni mpaka Makutano ya Mlingano, kilometa 39.5, economic potential ya barabara hii kwa Mkoa wa Tanga ni kubwa sana. Ninashangaa kuendelea kuona kwamba barabara hii kila siku inapigwa danadana. Kulikoni? Wanautakia mema kweli Mkoa wetu wa Tanga? Kwa sababu viwanda vyote vya saruji wanavyoviona Tanga vinategemea barabara hii. The best limestone in Sub-Saharan African Countries inatoka katika barabara hii na ni kilometa fupi sana, 39.5. Kulikoni isijengwe kwa kiwango cha lami? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, barabara hii licha ya kwamba ina economic potential kubwa katika Mkoa wetu wa Tanga lakini bado inaweza kuondosha msongamano wa Barabara ya Tanga – Segera ambayo sasa imeshazidiwa, kwa sababu hii inaweza ikawa ni bypass nzuri inayounganisha barabara kuu mbili; inaunganisha Tanga – Hororo kutoka Makutano ya Kiomoni na inaunganisha Tanga – Segera katika Makutano ya Mlingano. Barabara hii ni potential, ni Tanga bypass ambapo mtu anayetaka kwenda Mkinga akiwa anatokea Segera hana sababu ya kuingia Tanga Jiji, anaweza akapiga border akatokea zake Mkinga. Hali kadhalika anayetokea Mkinga kwenda Segera, hana sababu ya kuingia Tanga Jiji, anapiga kona anatokea zake Muheza mbele kwa mbele. Barabara hii ina umuhimu wa aina yake. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, viwanda vyote hivi vya saruji, viwanda wa liemba ambavyo viko pale, kwa nini hatuwatendei haki hata wafanyabiashara wakubwa ambao wapo ukanda huu? Fedha yote ya Mkoa wa Tanga, tunapoizungumzia Tanga Jiji inatoka kwenye ukanda huu kwa sababu ya saruji iliyopo pale na viwanda vile. Maana yake ni kwamba tunachelewesha hata wadau wengine wanaotamani kuja kufanya shughuli za kiuchumi kwenye Mkoa wa Tanga kwa sababu barabara ambayo ndiyo ina best limestone ipo nyuma na haiko katika kiwango cha lami mpaka leo. Hivi hatuutendei haki Mkoa wa Tanga na hatuwatendei haki Tanga Jiji. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaiomba sana Serikali, ninajua wameiweka kwenye kuifanyia upembuzi yakinifu na upembuzi wa kina; lakini this story is of very long time. Imechukua muda sana, inachosha kuisikia na tumechoka kusikia. We real need this road for sure kwa ajili ya maendeleo ya Tanga yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa ajili ya upanuzi wa Bandari ya Tanga na barabara hii na yenyewe connectivity yake inaweza ikatumika moja kwa moja mpaka Bandari ya Mkoa wa Tanga bila hata kuingia kule mbele. I am very sick and tired of this kwa kweli. Nimechoka kuisemea na ninaisemea kwa uchungu na ninaumia. Kulikoni mna hinder development ya Mkoa wa Tanga? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia alipozungumza kwamba anataka kuiona Tanga ambayo imeunganika kimiundombinu ni pamoja na barabara. Jamani ninaomba mtusaidie. Ninaona uchungu kusema kwamba ninaweza kushika shilingi ya shemeji yangu mpendwa, yaani kwa kweli ninaona shida, lakini kiukweli ninaumia, ninaumia, ninaumia and I am sick and tire of this road. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba niseme kwamba baada ya kusema hayo, ninaunga mkono hoja. Ahsante sana.